Pages

July 24, 2013

SIMLESA NA JUHUDI UTAFITI WA KILIMO HIFADHI CHA MIKUNDE KANDA YA MASHARIKI.


Mkuu wa wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro, Elias Tarimo akitoa maganda kwenye moja ya mahindi ili kuona ujazo wake katika shamba la mkulima la, Zuhura Geni kulia wakati wa sherehe ya sikukuu ya wakulima katika kijiji cha Mandela kuhusu kilimo mseto cha mahindi na mikunde juu ya kilimo hifadhi kupitia mradi wa Simlesa kwa ufadhi wa serikali ya Austaralia na Tanzania ikishirikiana na vituo vya utafiti vya kilimo Ilonga Morogoro na Selian Arusha ambazo sherehe hizo zilifanyika kijiji cha Mandela Kata ya Magole mwishoni mwa wiki mkoa wa Morogoro.
 
PICHA NA JUMAMTANDA.BLOG
 Mkuu wa wilaya akiangalia moja ya mahindi kutoka kwa mkulima.
Mkuu wa wilaya ya Kilosa, Elias Tarimo akisikiliza risala fupi ya utafiti wa kilimo mseto na mikunde kutoka kwa Mratibu waSemlesa, Bashir Makoko kulia wakati wa sherehe ya sikukuu ya wakulima katika kijiji cha Mandela kuhusu kilimo mseto cha mahindi na mikunde juu ya kilimo hifadhi kupitia mradi wa Simlesa kwa ufadhi wa serikali ya Austaralia na Tanzania ikishirikiana na vituo vya utafiti vya kilimo Ilonga Morogoro na Selian Arusha ambazo seherehe hizo zilifanyika kijiji cha Mandela kata ya Magole mwishoni mwa wiki mkoa wa Morogoro. 
Mtafiti kiongozi wa taasisi ya serikali katika mradi wa mifumo ya kilimo endelevu ya mahindi na mikunde mashariki na kusini na kusini mwa Afrika (SIMLESA) nchini,George Iranga kushoto akifafanua jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa,Elias Tarimo wakati wa sherehe ya sikukuu ya wakulima katika kijiji cha Mandela.  
 

 



Na Esther Mwimbula,Kilosa.
WAKULIMA wa vijiji vya Mandela, Magubwige, Mabana, Mfulu, Mdudu viliyopo kata ya magole tarafa ya magole wilayani kilosa mkoani Morogoro wametakiwa kulima kilimo cha hifadhi cha mahindi na mbaazi kutokana na zao hilo kuwa na uhakika wa soko ndani na nje ya nchi. 
Mtafiti wambegu za kilimo kutoka katika kituo cha utafiti cha chollima kilichopo dakawa mkoani humo Geoge Iranga alisema hayo alipokuwa akizungumza na wakulima hao na kudai kuwa imefikia wakati wakulima kulima kilimo ambacho kina manufaa kwao na kinakidhi matakwa ya wakulima.
 
Iranga alisema kuwaidadi kubwa ya wananchi waishio Tanzania wanategemea kilimo kwaajili ya kujikwamua kiuchumi hivyo wanatakiwa kulima kilimo ambacho kitawaingizia kipato ambacho kitawawezesha kujikwamua kiuchumi ikiwemo kuwalipia watoto wao karo za shule.
 
Aidha pia aliwataka wakulima hao kushiriki mafunzo mbalimbali ya kilimo cha mseto (SIMLESA)ambayo ambayo imekuwa ikiwawezesha wakulima kuweza kulima kilimo mseto ambacho kinamanufaa  kwa wakulima wadogo ambao wanategemea kilimo kama msingi wa maisha yao.
 
Wakizungumza kwa niaba ya wakulima wenzao Jumanne Bakari na Tatu Hamis walisema kuwa kilimo mseto kimewanufaisha kiuchumi na kujikwamua na janga la njaa ambalo limekuwa ni kero wa wakulima wadogo ambao wamekuwa wakitegemea kilimo katika shughuli za kilasiku.

Hivyo waliwaomba watafiti wa mbegu na kilimo kufika maeneo ya vijijini kutoa elimu ya kutosha ili waweze kulima kilimo cha tija na kuachana na kilimo cha mazoea.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...