Pages

July 2, 2013

KAMATI YA BUNGE YA ARDHI,MALIASILI NA MAZINGIRA YATUA NGORONGORO


Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro(NCAA),Bruno Kawasange(kulia) akifafanua jambo kwa wajumbe wa kamati ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Mazingira kwenye ziara ya kukagua miradi inayosimamiwa na NCAA.


Mwenyekiti wa Baraza la Wafugaji,Metui Ole Shaudo(shoto)akisalimiana na diwani wa Kata ya Nainokanoka ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro,Edward Maruo katikati ni Mbunge wa Longido,Michael Laizer

Mwenyekiti wa Kamati Bunge  ya Ardhi,Maliasili na Mazingira,James Lembeli akizungumza jambo wakati ziara ya kamati yake  katika Shule ya Sekondari Nainokanoka.



Mwenyekiti wa Kamati Bunge  ya Ardhi,Maliasili na Mazingira,James Lembeli akiipongeza NCAA kwa kujenga madarasa na madawati yenye ubora wa kiwango cha hali juu katika Shule ya Sekondari Nainokanoka.


Meneja Uhusiano wa NCAA,Adam Akyoo(shoto)akiteta jambo na Mbunge wa viti maalum,Ester Bulaya.


Wajumbe wa Kamati ya Ardhi,Nyumba na Mazingira na wananchi wakiondoka baada ya kukagua mabweni ya Shule ya Sekondari Nainokanoka iliyojengwa na NCAA.


Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Mbeya,Dk Mary Mwanjelwa akipata taswira na akinamama wa jamii ya wamasai wilayani Ngorongoro
A
Muonekano wa barabara inayotoka kwenye Bonde la Ngorongoro utakavyokua baada ya ujenzi wa kilometa 6 utakapokamilika


Wafanyakazi wa NCAA wakiwa kwenye mkutano na Kamati ya Ardhi,Maliasili na Mazingira

Meneja Uhusiano wa NCAA,Adam Akyoo akiangalia moja ya kipande cha tofali gumu yanayotumika kutengenezea barabara.Picha zote na www.rweyemamuinfo.blogspot.com

Na mwandishi wetu,Ngorongoro
Kamati ya bunge ya ardhi,maliasili na mazingira imeanza kukagua miradi mbalimbali inayosimamiwa na Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro(NCAA)huku wafanyakazi wakimshushia malalamiko mazito Mwenyekiti wa kamati hiyo James Lembeli.

Kati ya malalamiko hayo ni mishahara kiduchu wanayolipwa ukilinganisha na kazi wanazifanya huku wakidai kima cha chini cha mishahara wanayolipwa wafanyakazi wa Shiraka la Hifadhi za taifa nchini(Tanapa)kiko juu ukilinganisha na NCAA.

Mmoja wa wafanyakazi hao,Shema Mlela alidai licha ya NCAA kukisaidia kifedha chuo cha wanyamapori cha Mweka kilichopo mkoani Kilimanjaro,mishahara ya watumishi wa Chuo hicho iko juu ukiwamo wa Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo ukilinganisha na mshahara wa Mhifadhi Mkuu wa NCAA .

Amesema licha ya mapendekezo ya mishahara mipya kupelekwa wizarani bado wamegoma kuwaongezea mishahara hali inayowafanya kuishi maisha ya shida wakati mapato yanayoingia NCAA yamepanda kutoka bilioni 7 mwaka 2006 hadi bilioni 50 kwa sasa.

Kwa upande,Laban Moruo amedai kwa muda mrefu serikali imepuuza taasisi hiyo kwa kutomweka Mhifadhi mkuu badala yake wamekua wakiteuliwa watu wakukaimu nafasi hiyo bila sababu za msingi hali inayoshusha hari ya utendaji kwa watumishi. 

Mwenyeki wa kamati hiyo,James Lembeli amesema kitendo cha kutokuwalipa mishahara sitahili ni uonevu mkubwa ambao hawezi kuuvumia kwa wafanyakazi wanaofanya bidii kuongeza tija ya taasisi hiyo.

Katika hatua nyingine Lembeli akimea majungu miongoni mwa wafanyakazi hatua inayosababisha kuundwa tume baada ya tume ambazo hata hivyo zimekua hazina tija kwa NCAA.

"Kila wakati tume inakuja kuchunguza hapa,sioni umuhimu wa tume ambazo hazileti mrejesho kazi kubwa ni kufuja fedha zenu na ulaji tuu,nataka anayeunda tume atumie fedha zake na wala sio za NCAA aneundiwa tume.

Lembeli alikuja juu hatua ya serikali kuchota fedha kiasi cha Sh 600 milioni kupelekwa kwenye "Oparasheni"ambayo alidai ni ufisadi mkubwa na uachwe mara moja na kuwa hakuna oparasheni yeyote inayoendelea ya kupambana na ujangili ilihali kila siku Tembo wanauawa.



No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...