Muonekano wa mojawapo ya kumbi za Chuo cha Nelson Mandela,ArushaFilbert Rweyemamu,Arusha
Chuo Kikuu cha cha kiafrika cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela(AIST-NM)kimeanzisha utaratibu wa kuwa na wiki ya Nelson Mandela itakayokua ikitumika kuwakutanisha wasomi kujadili mambo mbalimbali ya namna ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia unavyoweza kuleta maendeleo ya kiuchumi katika bara la Afrika.
Katika mdahalo unaoendelea msemaji Mkuu,Profesa Calestous Juma kutoka Chuo
Kikuu cha Harvard,Marekani ambaye ni rais wa Kenya amesema Sayansi ikipewa kipaumbele inaweza kuleta maendeleo makubwa.
"Napenda kuwapongeza watanzania Rais Jakaya Kikwete anahamasisha matumizi ya Sayansi na Teknolojia ambayo baada ya muda mfupi Tanzania itakua imepiga hatua kubwa,"alisema
Makamu Mkuu wa Chuo hicho,Profesa Burton Mwamila amesema kila mwaka watakua na wiki ya Nelson Mandela ambaye taasisi hiyo ilianzishwa kwa mapendekezo yake.
Baadhi ya viongozi wanaohudhuria mdahalo huo ni Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Dk Florens Turuka ,Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Sayansi Mbeya(Mist)Profesa Joseph Msambichaka,Mkuu wa Chuo Dar es Salaam
Institute Technology(DIT)Profesa John Kondoro, Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu cha cha
kiafrika cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela(AIST-NM)Profesa Madundo
Mtambo ,Mkurugenzi wa Sayansi na Teknolojia,Profesa Evelyne Mbede jumuiya ya wanachuo hicho na wageni mbalimbali.
|
No comments:
Post a Comment