Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU)wakiimarisha ulinzi kwenye Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kaloleni wakati wa uchaguzi mdogo wa udiwani wa kata hiyo uliofanyika jana.Picha na Filbert Rweyemamu.
ARUSHA.
CHADEMA kimethibitisha umwamba wake katika siasa za Jimbo la Arusha Mjini, baada ya kutetea kwa kishindo kata zake nne kwenye uchaguzi mdogo wa udiwani uliofanyika jana.
Katika uchaguzi huo uliokuwa unasubiriwa kwa
hamu na ambao ulichukuliwa kama kipimo cha siasa za Arusha ambazo zimekuwa na
mvutano mkubwa, Chadema kiliongoza katikia vituo vyote 136 vya kupigia kura Kata
za Elerai, Kaloleni, Kimandolu na Themi.
Kata hizo zilikuwa wazi tangu mwaka 2011
baada ya Chadema kuwatimua wanachama wake waliokuwa madiwani Estomih
Mallah(Kimandolu), John Bayo (Elerai), Reuben Ngowi (Themi) na Charles Mpanda
(Kaloleni).
Matokeo
Katika matokeo yaliyotangazwa na Msimamizi
wa Uchaguzi Kata ya Elerai, Obedi Meng’oriki mshindi alikuwa Jeremiah Mpinga wa
Chadema aliyepata kura 2,047 dhidi ya 1,471 za Emmanuel Laizer wa CCM. Katika
Kata hiyo kulik
uwa na wagombea wengine ambao ni John Bayo (CUF; kura 302), Seif Shimba (CCK; kura 3) na Boisafi Shirima (TLP;1).
uwa na wagombea wengine ambao ni John Bayo (CUF; kura 302), Seif Shimba (CCK; kura 3) na Boisafi Shirima (TLP;1).
Katika Kata ya Themi, Kinabo Edmund wa
Chadema aliibuka na ushindi baada ya kupata kura kupata kura 674. Msimamizi wa
Uchaguzi Kata hiyo, Ezeka Mboya alisema Kinabo alifuatiwa na Victor Mkolwe
aliyepata kura 326 na Lobora Ndarpoi wa CUF alipata kura
307.
Kata ya Kaloleni, Msimamizi wa Uchaguzi,
Anna Ledisa alimtangaza Kessi Lewi wa Chadema kuwa mshindi kwa kura 1,470 dhidi
ya Emmanuel Mliari wa CCM aliyepata kura 330 na Abbas Mkindi wa CUF aliyepata
kura 275 na Ngilishi Pauli wa Demokrasia Makini aliyeambulia kura
mbili.
Kata ya Kimandolu, Msimamizi wa Uchaguzi,
Suleiman Kilingo alimtangaza Mchungaji Rayson Ngowi wa Chadema kuwa mshindi kwa
kura 2,761 na kumshinda Edna Saul wa CCM aliyepata kura 1,163. Kwa matokeo hayo,
Chadema sasa kimefikisha madiwani 12 wakati CCM kimebakiwa na kumi na moja na
TLP kina wawili.
Ushindi huo wa Chadema una athari kwa nafasi
ya Meya wa Jiji la Arusha, Gaudence Lyimo kwani CCM kina wajumbe 14 tu kwenye
Baraza la Madiwani, TLP wawili wakati Chadema sasa kimefikisha 15. Wabunge wa
majimbo na wale wa viti maalumu pia ni madiwani.
Aidha, Chadema kina nafasi ya kuongeza kiti
kingine cha udiwani kwani Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kinatarajiwa kuitisha
uchaguzi mdogo Kata ya Sombetini.
Mkurugenzi wa NEC, Julius Malaba alimwambia
mwandishi wetu kuwa tume yake inatarajia kuitisha uchaguzi mdogo hivi karibuni
baada ya kata hiyo kutangazwa wazi na Ofisi ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, Tamisemi.
Malaba alisema uchaguzi huo utaitishwa baada
ya aliyekuwa Diwani wake, Alphonce Mawazo kujitoa CCM na kujiunga na Chadema
hali inayokifanya chama tawala kuwa katika wakati mgumu kukitetea kiti hicho.
CHANZO MWANANCHI.
No comments:
Post a Comment