Kama kawaida maeneo kama haya maakuli ni sehemu muhimu sana hayawezi kuwa mbali hapa wahudumu wakiandaa sahani
Na Mwandishi Wetu,Arusha Wanafamilia wa Chuo cha Ufundi Arusha leo wamekua na siku ya kuburudika pamoja kwa kushiriki michezo mbalimbali iliyofanyika katika viwanja vya chuo hicho.
Mkuu wa Chuo hicho,Dr Richard Masika amesema siku hii inawapa nafasi wanafamilia kubadilishana mawazo,kujumuika kwenye michezo ya aina mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu,mchezo wa Netball,Vollebal,kukimbiza kuku,kuvuta kamba nk ili kuwapa nafasi ya kuimarisha afya zao.
Amesema fursa hii ni pekee kwa wanafamilia hao kuboresha mahusiano yao na wale walikosena kusameana na kuanza upya lengo likiwa kukuza umoja miongoni mwao. |
No comments:
Post a Comment