Pages

May 7, 2013

VIONGOZI ZAIDI WATEMBELEA MAJERUHI WA MABOMU,WALAANI WALIOTEKELEZA KITENDO HICHO,WASISITIZA WAHALIFU KUKAMATWA.

Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzaibar(SMZ)akizungumza na waandishi wa habari leo na kulaani kitendo cha ulipuaji wa Kanisa katoliki la Olasiti Jijini Arusha na kusema tukio hilo sio la kisiasa bali limefanywa na watu waovu wanaotaka kuchochea mifarakanokatika jamii ya watanzania na kutaka wakamatwe na kufikishwa kwenye mkono wa dola

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Idd akimsikiliza Cyprian ambaye mtoto wake Derick amelazwa kufuatia ulipuaji wa mabomu hayo

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akitoa shukrani kwa Mamlaka ya Hifadhi nchini(Tanapa)kwa msaada walioutoa wa vifaa vya matibabu wenye thamani ya Tsh 23 milioni kwa hospitali ya Mount Meru

Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo(kushoto) akitoa taarifa za kushikiliwa watuhumiwa 10 wanadhaniwa kuhusika na tukio la ulipuaji Kanisa,wengine ni Waziri Mkuu mstaafu,Edward Lowasa,Waziri wa nchi(mahusiano)Stephen Wasira,Naibu Waziri wa Ardhi,\nyumba na Maendeleo ya Makazi,Godluck Ole Medeye na Waziri Mkuu,Mizengo Pinda

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,lazaro Nyalandu akimjulia hali Regina Frederick aliyelazwa kwenye hospitali ya St.Elizabeth,kushoto ni mganga mkuu wa hospitali hiyo,Thomas Kwayu

Wakazi wa Arusha wakiingia kwenye hospitali ya mkoa wa Arusha,Mount Meru kuwajulia hali ndugu zao waliopatwa na janga la kupigwa mabomu kanisani

Jopo la waandishi wa habari kutoka vyobo mbalimbali vya habari mkoani Arusha wakiwa kwenye hospitali ya Mount Meru tayari kukusanya habari na kuujulisha umma kinachoendelea juu ya tukio la ulipuaji Kanisa Katoliki Parokia ya Olasiti jijini Arusha
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii akizungumza na wadau wa sekta ya utalii ambao pamoja na mambo mengine wamekubali kugharamia madaktari bingwa kusaidiana na waliopo kutoa huduma kwa majeruhi wa mabomu

Afisa wa shirika la Hifadhi za Taifa(Tanapa)Nuhu Amiri akiteremsha vifaa vya tiba vilivyotolewa na shirika hilo kuwasaidia wahanga wa mabomu
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii akiongoza kikao cha wadau wa kusaidia wahanga wa mabomu

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...