Pages

May 13, 2013

MTUHUMIWA WA UGAIDI ARUSHA AFIKISHWA KIZIMBANI CHINI YA ULINZI MKALI


Na mwandishi maalum
Mtuhumiwa wa kurusha Bomu kwenye Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph,Parokia ya Olasiti ,Jimbo Kuu la Arusha,Victor Ambrose Calist amefikishwa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la Polisi kwenye  Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ,mbele ya Hakimu Mkazi,Devota Kamuzora leo.
Ambrose amesomewa  mashtaka 21 ya kuua na kujaribu kuua  wakati wa uzinduzi wa kanisa hilo ambao mgeni rasmi alikua Balozi wa Vatican nchini,Askofu Mkuu,Fransisco Padilla  ambaye alikuwa na mwenyeji wake Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Arusha,Josephat Lebulu.
Katika hatua nyingine Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha,Liberatus Sabas amesema kuwa watuhumiwa watatu raia wa United Arab Emirates(UAE)Abdul Aziz Mubrak(30)ambaye ni mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato ,Fouad Saleem Ahmed Hareez Al Mahri(29)Saeed Abdulla Saad(28)ambaye ni askari Polisi  na raia mmoja wa Saudia Arabia,Al Mahri Saeed Mohseens(29)
Sabas amesema watuhumiwa wengine bado wanahojiwa kuona namna gani wanahusika na kitendo hicho cha kigaidi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...