Matukio
ya Kisiasa
Mgombea
chama cha SPD Steinbrueck ateua kikosi cha kampeni
Kiongozi wa chama cha upinzani
nchini Ujerumani SPD Steinbrueck amejaribu kuiweka sawa kampeni
yake inayoyumba yumba katika mkakati wa kupambana na kansela Angela Merkel
katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
Mawaziri watatu kivuli wa chama cha
upinzani cha Social Democratic SPD waliomo katika kikosi hicho watashikilia
nyadhifa katika masuala ya ndani na sheria, sera za internet na kazi pamoja na
masuala ya kijamii.
Lakini wajumbe wengi wa kundi hilo
hata hivyo bado hawajatajwa hadharani. Wajumbe hao watatu waliotajwa leo
walithibitishwa baada ya majina yao kuvuja katika vyombo vya habari na
kulazimisha kutangazwa rasmi siku moja kabla ya siku rasmi ya kufanya hivyo.
Mwenyekiti wa chama cha SPD Sigmar
Gabriel
Uchunguzi wa maoni
Zaidi ya hayo , uchunguzi wa maoni
ya wapiga kura unaonesha kuwa Merkel bado yuko mbele ya Steinbrueck , wakati
wapiga kura walipoulizwa kuwa nani wanampendelea kuiongoza nchi yao.
Hii inafuatia kile Wajerumani wengi
wanakiona kuwa ni uwezo wa kansela Merkel kulishughulikia suala la muda mrefu
la mzozo wa madeni katika mataifa yanayotumia sarafu ya euro.
Jukwaa analotumia Steinbrueck katika
uchaguzi huu, ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa mshahara wa kima cha chini na
kuwatoza kodi watu wenye kipato cha juu, linaonekana kutofanya chochote
kupindua majaaliwa ya chama cha SPD katika uchaguzi huu.
SPD na maoni ya wapiga kura
Chama kinaendelea kubakia katika
kiwango cha asilimia 24 ya kura kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni ya wapiga
kura.
Lakini serikali za Ujerumani
zinaundwa kwa kuungwa mkono chama katika uchaguzi badala ya kura ya taifa
kumchagua kiongozi.
Uchunguzi wa maoni wa hivi karibuni
unaonesha kuwa chama cha kansela Angela Merkel cha Christian Democratic kina
nafasi ya kuibuka na asilimia 40 ya kura, ambazo zitakifanya kuwa ni kundi
kubwa katika bunge, katika uchaguzi wa hapo Septemba.
No comments:
Post a Comment