Pages

May 14, 2013

MAADHIMISHO YA SIKU YA WAUGUZI ARUSHA LEO YAFANA,WATAKIWA KUACHA KAULI ZISIZOFAA KWA WAGONJWA

Wauguzi kutoka hospitali mbalimbali jijini Arusha wakiserebuka wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wauguzi duniani ilifanyika leo katika hospitali ya Selian(ALMC)

Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Centre(ALMC)akisoma hotuma yake

Wauguzi wakiwasha mishumaa yao wakati maadhimisho hayo

Sanaa ya maigizo ilipamba maadhimisho hayo

Wauguzi waliamua kukumbukia enzi zile kuimba mashairi
Wauguzi wakila kiapo cha utii na uaminifu wakutokutoa siri za wagonjwa na kutokufanya vitendo viovu leo


Na mwandishi wetu,Arusha
Wauguzi mkoa wa Arusha wameadhimisha siku ya wauguzi duniani leo kwa shamrashamra nyingi kwenye viwanja vya hospitali ya Arusha Lutheran Medical Center(ALMC) kwa kushirikisha wauguzi kutoka hospitali zilizopo jijini hapa.

Muuguzi Mkuu wa Jiji la Arusha,Jane Barakururiza alisema maadhimisho hayo ni muhimu sana kwao kutokana na wajibu wao wa kuwahudumia wagonjwa na kuwasaidia madaktari koukoa maisha ya wagonjwa.

Maadhimisho yaho yalianzia kweny hospitali ya AICC kwa maandamano na kupitia barabara ya Sokoine,Makongoro hadi hospitali ya Selian

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...