Na Filbert Rweyemamu,Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo amewataka wazazi
kutumia wiki ya chanjo kuwapeleka watoto kupewa matone dhidi ya magonjwa
mbalimbali ukiwemp wa Polio.
Ametoa kauli hiyo leo wakati wa uzinduzi wa chanjo watoto
walio chini ya umri wa miaka mitano mkoa wa Arusha katika Kijiji cha Mbuyuni
Kata ya Oljoro,wilayani Arumeru
Amewataka viongozi wa vijiji kuweka sheria ndigondogo
zitakazowabana wananchi ambao watakaidi kuwapeleka watoto kupata chanjo hiyo
muhimu inayogharimiwa na serikali kwa wananchi wake.
Mulongo amesema kutokana na chanjo hizo kutolewa baadhi ya
magonjwa yametoweka kabisa na zilizokuwa Wodi za magonjwa hayo katika hospitali
ya mkoa ya Mount Meru zinatumika kwa mambo mengine.
Awali Mganga Mkuu wa mkoa wa Arusha,Frida Mokiti alisema
mwitikio wa chanjo kwa mkoa wa Arusha unaridhisha kutokana na takwimu za mwaka
jana kuwa miongoni mwa mikoa minne iliyofanya vizuri kitaifa huku wilaya ya
Ngorongoro ikivuka asilimia 100.
Amesema utoaji wa chanjo hizo ni mkakati wa wizara ya Afya
na Ustawi wa Jamii kuhakikisha nchi inafikia lengo namba nnela millennia la
kupunguza vifo vya watoto kwa theluthi mbili sanjari na kuzitaka halmashauri
zote kufanikisha zoezi hilo kwa kiwango cha asilimia 95 kwa kila chanjo.
Kauli mbiu ya wiki ya chanjo kwa mwaka huu ni "Okoa Maisha.Kinga Ulemavu.Toa Chanjo
Kauli mbiu ya wiki ya chanjo kwa mwaka huu ni "Okoa Maisha.Kinga Ulemavu.Toa Chanjo
No comments:
Post a Comment