Na Filbert Rweyemamu,Babati
MKUU Mkoa wa Manyara,Eraston Mbwilo amesema kutokana na wilaya za Mbulu na Hanang kuwa na migogoro mingi ya ardhi kuna sababu ya mamlaka husika kuajiri wenyeviti wa mabaraza ya ardhi katika wilaya hizo badala ya kuja makao makuu ya mkoa mjini Babati .
Pia alisema katika wilaya za Simanjiro na Kiteto yupo mwenyekiti wa baraza la ardhi anaeishi Simanjiro wakati migogoro mingi iko Kiteto hivyo kumgharimu zaidi kwenda huko na wakati mwingine huleta malalamiko kwa wananchi.
Akizungumza mbele ya Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Profesa Anna Tibaijuka alisema kuna uwezekano mkubwa kuwa mkoa wa Manyara unaongoza kwa migogoro ya ardhi ukilinganisha na kwingine.
“Nakumbuka miaka ya nyuma nimewahi kuwa Mkuu wa wilaya ya Mbulu wakati huo kati ya wananchi 40 waliokuwa wanafika kuniona,wananchi wanne tu ndio wangezungumza mambo yasiyohusu migogoro ya ardhi hivyo naomba uone umuhimu wa wilaya hizo kupata wenyeviti watakaokuwa na makazi yao huko ili kuwapunguzia gharama ya kuja Babati,”alisema Mbwilo
Kwa upande wake,Profesa Tibaijuka alizitaka mamlaka husika kuwalipa wananchi fidia zinazoendana na bei ya soka kwenye maeneo wanayotaka kuyachua kutoka kwa wawekezaji au wananchi kwa ujumla ili kuepusha matatizo ya mara kwa mara na wananchi.
Alisema katika mipango ya halmashauri na mkoa wanatakiwa kabla ya kuyapangia matumizi maeneo yanayokaliwa na wananchi waandae fidia inayolingana na bei soko na walipe kwa wakati kwani muda wa miaka mine baada ya tathmini kufanyika malipo hayatua halali tathmini inatakiwa kufanyika upya.
Profesa Tibaijuka alitoa kauli hiyo baada ya Mkuu wa mkoa kumweleza kuwa,Jeshi la Polisi kwenye mkoa huo limeshindwa kuanza kujenga makao yao makuu kutokana na fedha zilitumwa halmashauri ili kuwalipa fidia wananchi kutokulipwa kwa wakati na kudai malipo zaidi.
“Ni vizuri mkafahamu sheria inasemaje ikishapita miaka minne tangu tathmini imefanyika na wanaotakiwa kulipwa fidia hawakulipwa,tathmini ifanywe upya sasa hili sio zuri kwasababu litaigharimu zaidi fedha serikali za wananchi ambazo zingetumika kwenye mambo mengine ya maendeleo,”alisema
Alimtaka Mkurugenzi wa Mji huo kuandaa ramani itakayosaidia mji kuwa katika mpangilio badala ya kuwaacha wananchi wajenge makazi holela ambayo baadaye ni gharama kuupanga mji.
|
March 15, 2013
MANYARA YAONGOZA KWA MIGOGORO YA ARDHI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment