Uwanja wa kimataifa wa AFCON unaojengwa jijini Arusha.
Filbert Rweyemamu,Arusha
Kamati ya Usalama ya Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) imetoa wito kwa vyombo vyote vya ulinzi na taasisi za serikali kudumisha moyo wa ushirikiano uliojengwa huku ikisisitiza kuwa hakuna taasisi moja inayoweza kujitegemea kulinda matukio makubwa ya kimataifa.
Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Usalama ambaye ni Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,Jumanne Mulilo wakati wa kufunga warsha ya kitaifa jijini Arusha iliyoandaliwa na Tume ya Nguvu za AtomiTanzania (TAEC) na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Nyuklia (IAEA), iliyolenga kujenga mifumo ya usalama wa nyuklia na mionzi kuelekea michuano hiyo.
Mulilo amesema Kamati hiyo ya Usalama alipongeza mafanikio makubwa yaliyopatikana kwenye zoezi la kiutendaji la vitendo lililofanyika alhamisi katika uwanja mpya wa mpira wa miguu.
Zoezi hilo lilihusisha uigizaji wa kutafuta vyanzo vya mionzi vilivyofichwa, kuwafanyia ukaguzi wa kina watazamaji milangoni, kufanya upekuzi maeneo ya kimkakati na kulinda njia maalum za wageni mashuhuri.
"Zoezi hili limetuonyesha kwa vitendo namna maandalizi, watumishi waliofunzwa vizuri, mawasiliano ya haraka na mifumo ya pamoja ya uongozi na uratibu inavyoweza kuzuia majanga makubwa," amesema Mulilo
Aliongeza kuwa kumalizika kwa warsha hiyo si mwisho wa kazi, bali ni mwanzo wa safari ndefu ya kugeuza maarifa hayo kuwa hatua madhubuti ikiwemo kukamilisha dhana ya uendeshaji na kubaini mahitaji halisi ya vifaa vya kiutendaji.
Kamanda Mulilo amesema kuwa nchi sasa inajifahamu vizuri kiuwezo kuliko kabla ya warsha hiyo na iko tayari kutathmini mapema viashiria vyote vya vihatarishi vya kiusalama.
‘Kiusalama tumejipanga,kwenye michuano ya AFCON iliyofanyika Morocco na Kombe la Dunia lililomalizika nchini Marekani tulituma watu wetu kujifunza mbinu za kiusalama kwenye mikusanyiko ya watu wengi,”amesema Mulilo
Kamati hiyo imeahidi kuendelea kufanya kazi bega kwa bega na TAEC ili
kuhakikisha hatua zote za usalama wa nyuklia zinaunganishwa kikamilifu kwenye
mpango mkuu wa usalama wa taifa wakati wa AFCON 2027.
Mbali na TAEC na wataalamu wa IAEA, taasisi zilizoshiriki mafunzo hayo ni
pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama, mamlaka za afya ya umma, dharura na
usimamizi wa matukio.
Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Usalama ambaye ni Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,Jumanne Mulilo wakati wa kufunga warsha ya kitaifa jijini Arusha iliyoandaliwa na Tume ya Nguvu za AtomiTanzania (TAEC) na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Nyuklia (IAEA).


إرسال تعليق