Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itazindua rasmi Awamu ya Pili ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC II) ikiwa ni hatua muhimu ya kuendelea kusogeza huduma za msaada wa kisheria, elimu ya sheria na upatikanaji wa haki karibu na wananchi wote nchini bila ubaguzi.
Kampeni hiyo ni utekelezaji wa maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, yanayolenga kuhakikisha kila mwananchi anapata haki kwa wakati, uelewa wa sheria na uwezo wa kutatua changamoto za kisheria zinazomkabili katika maisha ya kila siku.
Akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dodoma Waziri wa Katiba na Sheria, Juma Zuberi Homera amesema Awamu ya Pili ya kampeni hiyo imejengwa juu ya mafanikio ya awali yaliyopatikana katika Awamu ya Kwanza iliyotekelezwa kuanzia Aprili 2023 hadi Juni 2025 katika mikoa yote 31 ya Tanzania.

Alieleza kuwa kupitia kampeni hiyo wananchi wengi walifikishiwa huduma mbalimbali za kisheria zikiwemo elimu ya sheria, ushauri wa kisheria na usuluhishi wa migogoro, hatua iliyosaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza uelewa wa jamii kuhusu haki na wajibu wao.
Kwa upande wa Zanzibar, kampeni ya awali ilitekelezwa katika mikoa yote mitano ya Unguja na Pemba ambapo jumla ya wananchi 422,908 walinufaika na huduma hizo. Kati yao, wanaume walikuwa 213,723 na wanawake 209,185.

Mafanikio hayo yameelezwa kuwa ni ishara ya umuhimu wa huduma za msaada wa kisheria katika kuimarisha amani, kupunguza migogoro na kuongeza uelewa wa sheria katika jamii.
Kutokana na mafanikio hayo, Serikali imeamua kuendelea na Awamu ya Pili ya kampeni hii ambayo inalenga kuwafikia wananchi wengi zaidi, hususan walioko maeneo ya pembezoni na vijijini ambako upatikanaji wa huduma za kisheria bado ni changamoto.
Kupitia awamu hii mpya, wananchi watanufaika na huduma mbalimbali ikiwemo masuala ya ndoa na talaka, mirathi na wosia, migogoro ya ardhi, haki za watoto, ukatili wa kijinsia, haki za wafanyakazi, usuluhishi wa migogoro kwa njia mbadala pamoja na huduma za usajili wa matukio muhimu ya maisha na upatikanaji wa nyaraka muhimu za utambulisho.
Uzinduzi wa kitaifa wa Awamu ya Pili ya MSLAC unatarajiwa kufanyika tarehe 20 Juni 2026 katika Viwanja vya Maonesho Dole vilivyopo Wilaya ya Magharibi A, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Samia suluhu hasani na pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Hussein Ali Mwinyi atakuwepo pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali, taasisi za umma na binafsi, mashirika ya kiraia na wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Zanzibar.
Serikali imesema zaidi ya washiriki 15,000 wanatarajiwa kuhudhuria uzinduzi huo mkubwa, ambao pia utahusisha utoaji wa huduma kupitia mabanda maalumu katika wilaya za Mjini, Magharibi A na Magharibi B. Aidha, timu za wataalamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Kamisheni ya Ardhi, Jeshi la Polisi Zanzibar pamoja na Jumuiya ya Mawakili Zanzibar zitapita katika shehia mbalimbali kutoa elimu ya sheria, usuluhishi wa migogoro na huduma nyingine za kisheria kwa wananchi moja kwa moja.
Serikali imewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki uzinduzi huo na kunufaika na huduma zitakazotolewa, ikielezwa kuwa kampeni hiyo ni fursa muhimu ya kuongeza uelewa wa sheria, kupunguza migogoro ya kijamii na kuimarisha amani na utulivu nchini.

Aidha, imeelezwa kuwa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia inaendelea kuwa mfano wa ushirikiano imara kati ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuhakikisha haki inawafikia wananchi wote kwa usawa.

Post a Comment