Wananchi kata ya Magugu Wampongeza DC kwa Kutatua Mgogoro uliodumu miaka 20.

 

Wananchi wa kata ya Magugu  iliyopo Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara wamemahukuru Mkuu wa Wilaya hiyo kwa kufanisha kutatua mgogoro uliodumu zaidi ya miaka (20).

Katika mgogoro huo, ilibainika kuwa baadhi ya wananchi walikuwa wamevamia eneo la mwekezaji katika maeneo ya vijiji vya Malangi na Kirusix, ambapo walikuwa wamejenga nyumba za kudumu pamoja na kuweka makaburi.

Katika juhudi za kutatua mgogoro huo, Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya alimshauri mwekezaji kukata sehemu ya eneo lake, hususan maeneo ambayo tayari wananchi wengi walikuwa wamejenga, ikiwemo Malangi na Kirusix.

Mwekezaji alikubali ombi hilo na kuamua kuachia sehemu ya eneo lake ili wananchi waweze kuishi kihalali.

Aidha, Mheshimiwa DC aliwaelekeza maafisa ardhi kwenda uwandani kwa ajili ya kupima eneo hilo lililotolewa kwa wananchi ambapo ilikubaini ukubwa wake pamoja na kuweka mipaka rasmi.

Vilevile, wananchi wote waliokuwa wamejenga katika eneo la mwekezaji walielekezwa kupewa viwanja katika eneo hilo jipya lililotengwa na kisha kuhamia huko rasmi.

Kwa upande mwingine, Mheshimiwa DC aliwataka wananchi kuishi kwa amani na kushirikiana katika kulinda mali za mwekezaji ili kudumisha uhusiano mzuri na maendeleo endelevu katika eneo hilo.









Post a Comment

Previous Post Next Post