Raushan DesignShroff TemplatesMafiaXDesign

Rais Ndayishimiye Aonya Rwanda Kuhusu Jaribio Lolote la Kuvamia Burundi

 Kauli ya Rais wa Burundi,Meja Jenerali,Evareste Ndayishimiye ilichukuliwa kama jibu la kutokubaliana na utawala wa Rwanda.

 Rais Ndayishimiye alisema kuwa mchakato wa kuwakamata na kuwafungulia mashtaka viongozi wa waasi wa Red Tabara unaendelea, na serikali haina nia yoyote ya kufanya mazungumzo nao.


Aidha, Rais Ndayishimiye alisisitiza kuwa Burundi haina nia ya kuvamia nchi nyingine au kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine, akisema kuwa nchi yake inastahili heshima kama taifa lingine lolote. 

 "Hatutakubali kuchinjwa kama mbuzi, kama vile Wakongomani," alisema Rais Ndayishimiye, akionyesha wazi kuwa Burundi imejizatiti kujilinda dhidi ya uvamizi wowote kutoka nje.

Ushirikiano wa kijeshi na kiusalama kati ya Burundi na Rwanda bado ni jambo linalozungumziwa kwa umakini, huku viongozi wa mataifa haya mawili wakikubaliana kuwa mzozo katika Mashariki mwa DRC ni moja ya masuala yanayohitaji majadiliano ya kina ili kuhakikisha usalama wa mipaka yao na kuepusha hatari za vita vya kikanda.

Post a Comment

Previous Post Next Post