Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema Serikali Mkoani humo
haijawakataa wadau wa Afya kutoka katika Mashirika mbalimbali ya Kitaifa
na Kimataifa wanaofanya kazi mbalimbali katika kuunga mkono juhudi za
Serikali kwenye Sekta ya Afya, bali inatambua mchango wao na inawaomba
kufanya kazi kwa kuzingatia vipaumbele vya Kitaifa na Mkoa kwenye Sekta
ya Afya.
Mtaka
ameyasema hayo katika mazungumzo maalum na waandishi wa Habari wakati
alipokuwa akifafanua kauli aliyoitoa katika kikao kilichofanyika
Februari 25 na 26 Mjini Bariadi kati ya Viongozi wa Mkoa huo na Wadau
Afya mkoani humo ya kuwataka kuelekeza zaidi fedha zao katika kujibu
mahitaji ya wananchi kwenye Afya badala ya semina na mafunzo kwa
watumishi.
Amesema
Serikali inatambua mchango wa Mashirika na wadau wa Afya Mkoani humo
kutokana na mambo waliyoyafanya kuunga mkono Serikali kutatatua
changamoto mbalimbali za Sekta ya Afya, ikiwa ni pamoja na kutoa magari,
kujenga majengo ya upasuaji katika baadhi ya Vituo vya Afya na
kuwajengea uwezo watumishi wa afya.
Ameongeza
kuwa pamoja na michango hiyo Mashirika mengi yanayofanya kazi Mkoani
Simiyu katika Sekta ya Afya yameonekana kujikita zaidi katika kutoa
fedha nyingi kwa ajili ya semina na mafunzo kwa watumishi wa Afya ,
badala ya kusaidia katika kutatua changamoto ambazo ni vipaumbele vya
Kitaifa na Mkoa pia katika Sekta ya Afya.
Aidha.
Mtaka amebainisha kuwa Vipaumbele vya Kitaifa na Mkoa katika Sekta ya
Afya ni pamoja na Ujenzi wa Miundombinu ya Afya ambayo ni majengo ya
zahanati, vituo vya afya, vyumba vya upasuaji, hospitali), Vifaa pamoja
na vifaa tiba, ambapo alieleza kuwa Mkoa huo una upungufu wa Hospitali
ya Mkoa, Hospitali mbili za Wilaya, Vituo vya Afya 112 na Zahanati 291.
“Tumepitia
bajeti za mashirika haya 11 kwa ujumla wake mwaka 2018 yatatumia zaidi
ya shilingi bilioni 21, hizi ni fedha nyingi ambazo kama zitafanya kazi
inayoonekana huduma za Afya ndani ya mkoa zitaimarika, changamoto kubwa
ambayo mimi kama mkuu wa mkoa na viongozi wenzangu tumeiona ni fedha
nyingi kati ya hizo kuelekezwa kwenye mafunzo ya watumishi wa afya”
alisema
“Kwanza
nimeyaomba mashirika yanayofanya kazi za Sekta ya Afya ndani ya Mkoa
kila moja kuonesha kazi wanazofanya, pili natoa wito kwa mashirika haya
kuelekeza fedha nyingi kwenye kuongeza idadi ya vituo vya afya,
zahanati, vifaa na vifaa tiba ili tunapojenga uwezo kwa watumishi wetu
wa Afya wawe na mahali pa kwenda kufanyia kazi mafunzo wanayopata”
alisisitiza Mtaka
Ameongeza
kuwa Ofisi yake imeandika barua Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ili Viongozi kutoka Wizara hizo
mbili wakutanishwe pamoja na Viongozi wa Wizara ya Afya na Viongozi wa
Mkoa wa Simiyu kwa lengo la kujadili na kuchambua tija ya fedha za
wadau/mashirika hayo kwenye Sekta ya Afya.
Mmoja
wa wadau hao Mwakilishi kutoka Shirika la Mkapa Foundation Bi.Adeline
Saguti akichangia hoja katika kikao chao na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu
alisema Wadau wa Afya Mkoani humo wameahidi kushirikiana na Mkoa huo
kufanyia kazi maeneo yenye uhitaji katika Sekta ya Afya.
Wadau
wa Afya (mashirika ya ndani na nje ya nchi) wanaofanya kazi na mkoa wa
Simiyu ni pamoja na AMREF, AGPAHI, CUAMM, UNFPA, Mkapa Foundation,
AMERICARE, Red Cross, ICAP, TAMA, INTRAHELTH, WORD VISION na BORESHA
AFYA.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) ofisini kwake Machi O2, 2018 Mjini Bariadi
No comments:
Post a Comment