Waziri wa Mifugo na
Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina (mwenye koti jekundu)akimsikiliza
Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, Hamad Rashid Muhamed ofisini kwake leo wakati alipofanya
ziara ya kikazi katika Kisiwa Unguja. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa
Mamlakaya
Kusimamia Uvuvi
wa Bahari Kuu(DSFA),Hosea Gonza Mbilinyi. (Picha na John
Mapepele)
Waziri wa Kilimo, Maliasili,
Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hamad Rashid Muhamed(mwenye
suti nyeupe) kushoto kwake ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga
Joelson Mpina (mwenye koti jekundu) na kulia kwake ni Katibu Mkuu Uvuvi
Tanzania Bara Dkt. Yohana Budeba wakiwa katika picha ya pamoja
na Wakurugenzi na Watendaji wa Sekta ya Uvuvi mara baada ya Waziri Mpina
na Watendaji wake kuwasili leo Unguja kwa ziara ya kikazi. (Picha na
John Mapepele)
Baadhi ya watumishi
wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu(DSFA) wakimsikiliza
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina (hayupo
pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika leo katika ofisi ya Mamlaka
hiyo Fumba katika kisiwa cha Unguja leo. (Picha na John
Mapepele)
Kiongozi wa Kampuni
ya Linghang kutoka China inayoshughulika na uendelezaji
wa Utalii wa Zanzibar nchini china Tom Zhang (katikati) akiwa
na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, Hamad Rashid Muhamed(mwenye suti nyeupe) kushoto kwake ni
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina (mwenye koti jekundu)
wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Waziri Mpina na Watendaji
wake kuwasili leo Unguja kwa ziara ya kikazi. (Picha na John
Mapepele)
Na John
Mapepele
Serikali imezipiga
faini ya bilioni kumi na tisa meli 19 ikiwa
ni shilingi bilioni moja kwa kila meli na kuamuliwa kulipa faini hiyo
ndani ya wiki mbili kwa kukiuka kanuni ya 10 ikisomeka pamoja na kanuni
ya 68 ya kanuni za uvuvi wa Bahari Kuu za mwaka 2009 pamoja na marekebisho
yake ya mwaka 2016 kwa kutoripoti katika bandari Dar es Salaam, Zanzibar,
Mtwara ama Tanga kwa ajili ya ukaguzi kabla ya kutoka katika bahari
kuu ya Tanzania.
Akizungumza na
Waandishi wa Habari, katika Ofisi za Mamlaka ya Uvuvi
wa Bahari Kuu zilizopo Fumba kisiwani Unguja, Waziri wa Mifugo
na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina amesema pamoja na meli hizo kuamriwa
kulipa faini ya Shillingi Billioni moja (Tshs. 1,000,000,000) kila moja
zinatakiwa kurejea katika bandari za Tanzania kwa ajili ya ukaguzi
kwa kuwa leseni zao bado hazijaisha muda wake hadi sasa ili kubaini
thamani halisi ya kiasi cha fedha zitakazotozwa kwa ajili ya samaki
waliovuliwa bila kukusudia(Bycatch).
Aidha Mpina amesema
meli hizi zimetakiwa kuilipa Tanzania kiwango
cha pesa kwa mujibu wa soko la kimataifa kutokana na kuondoka na Bycatch
waliyoripoti kuwa wanayo kabla ya kutoroka.
Waziri Mpina
amemuagiza Katibu Mkuu Uvuvi, Dkt. Yohana Budeba
kuiamru Mamlaka ya uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA) iwaandikie notisi wahusika
wa meli hizi kuwajulisha kuhusiana na maamuzi haya pia kuwajulisha Kamisheni
ya Jodari kwenye Bahari ya Hindi, (IOTC) kuhusiana na hatua zilizochukuliwa
na Tanzania dhidi ya meli hizo ili isaidie kuwabaini na kuwachukulia
sheria kwa mujibu wa Sheria husika.
Aidha imeamriwa kwamba
Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu pia iandae barua/
andiko kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili aweze kuiandikia
Barua Wizara ya Mambo ya Nje kwa lengo la kuwasiliana na Flag States
(Mataifa ambayo meli hizi zimesajiliwa) ili kuwajulisha makosa yaliyotendwa
na meli husika pamoja na hatua ambazo Tanzania imechukua. Amesema meli
zote zilizotoroka zimesajiliwa nchini China.
Wakati huo huo Waziri
Mpina amesema meli ya Tai Hong 1 imekiuka Kifungu
cha 18 cha Sheria ya uvuvi wa Bahari kuu No. 1 ya Mwaka 1998 na marekebisho
yake ya mwaka 2007 pamoja na Kanuni ya 66 ya kanuni za uvuvi wa Bahari
kuu za Mwaka 2009 na marekebisho yake ya mwaka 2016 kwa kukutwa na mapezi
ya papa yasiyoendana na miili iliyokutwa kwenye meli hiyo baada ya kukaguliwa
katika bandari ya Dar es Salaam mnamo tarehe
25/01/2018-27/01/2018.
Pia meli hii
imebainika kukiuka kanuni ya 10 ikisomeka pamoja na kanuni
ya 68 ya kanuni za uvuvi wa Bahari Kuu za mwaka 2009 pamoja na marekebisho
yake ya mwaka 2016 kwa kuhaulisha mabaharia kutoka kwenye meli nyingine
ambao idadi yao ilikuwa mabaharia 10.
Aidha meli hii pamoja
na kukutwa na makosa hayo iliondoka nchini bila
kufuata taratibu zinazotakiwa kwa mujibu wa vifungu tajwa hapo
juu.
Kutokana na makosa
hayo imeamriwa na Mamlaka ya Bahari kuu (DEEP SEA
FISHING AUTHORITY) kulipa jumla ya faini ya Shillingi Billion moja (Tshs.
1,000,000,000) ambapo Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu itawasilisha notisi
ya adhabu hii kwa wahusika wa Meli hii ya TAI HONG
1.
Mbali na Tai Hong 1
Mpina amezitaja Meli hizo zilizopigwa faini ya
Bilioni moja kila moja kuwa ni pamoja na TAI HONG NO2 yenye namba
ya leseni TZ/DSFA/EEZ/453, TAI HONG 8 yenye namba ya leseni
TZ/DSFA/EEZ/454,
,TAI XIANG 2 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/455, TAI XIANG
5 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/456, TAI XIANG 1 yenye
namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/457, TAI XIANG 8 yenye namba ya leseni
TZ/DSFA/EEZ/458 na TAI XIANG 9 yenye namba ya leseni
TZ/DSFA/EEZ/459.
Meli nyingine ni TAI
XIANG 10 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/460,
TAI XIANG 7 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/461, TAI XIANG 6
yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/462, TAI HONG 6 yenye
namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/463, TAI HONG 7 yenye namba
ya leseni TZ/DSFA/EEZ/464, XIN SHIJI 81 yenye namba ya leseni
TZ/DSFA/EEZ/466, XIN SHIJI 82 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/467,
XIN SHIJI 83 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/468, XIN SHIJI
86 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/470, XIN SHIJI 72 yenye
namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/471, XIN SHIJI 76 yenye namba ya leseni
TZ/DSFA/EEZ/472 na JIN SHENG 1 yenye namba ya leseni
TZ/DSFA/EEZ/473.
Naye Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Yohana Budeba amewataka
wawekezaji kwenye bahari ya Tanzania kuwa waaminifu na kuzingatia
masharti na taratibu za kisheria ili nchi na wawekezaji waweze
kunufaika.
“Taratibu zipo wazi ni
muhimu kuzinangatia sheria namna
nyingine tutaendelea kusimamia sheria za nchi yetu kwa faida ya sasa
na vizazi vya baadaye” Alisisitiza Dkt.
Budeba
Amesema hatua
iliyochukuliwa na Serikali ya kuzipiga faini
meli hizo ni somo kwa meli nyingine na kwamba Serikali itaendelea kuchukua
hatua kali kwa yoyote atakayebainika kutenda makosa ya uvuvi
haramu katika bahari na maziwani.
Aidha amesema Serikali
ipo tayari kufanya biashara na mtu yoyote
ambaye atazingatia masharti ya nchi, na kwamba taifa linajipanga ili
kuwa na makampuni yake ya TAFICO na ZAFICO yatakayoshuhulika na uvuvi
ili kunufaika na raslimali za uvuvi kama ambavyo inafanyika katika nchi
mbalimbali duniani.
Amesema hatua hiyo
itasaidia kukuza ajira kwa wananchi, uchumi wan
chi na kuanzisha viwanda vya kuchakata samaki na mazao
yake.
Aliwashukuru
wadau wote wanaoshiriki kwenye mapambano ya uvuvi
ambapo kipekee alilishukuru shirika lisilo la kiselikali la Sea worrior
kwa kutoa mchango mkubwa kwenye operesheni Jodari ambayo imefanywa
na wadau mbalimbali nchini.
No comments:
Post a Comment