Afisa
Mkuu wa Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika kutoka Manispaa ya
Kinondoni,Saleh Hijja Mohamed (aliyesimama) akizungumza kabla ya
kumalizika kwa semina ya siku tatu ya mafunzo ya uongozi kwa walimu wa
shule za msingi na sekondari wa Jiji la Dar es Salaam leo. Semina hiyo
imefanyika katika Kituo cha Walimu cha Mzimuni kilichopo Magomeni
Mapipa. Kulia wanaoshuhudia ni Afisa Mkuu wa Miradi wa Shirika lisilo la
Kiserikali la British Council,Atiya Sumar na Meneja Miradi wa Shirika
hilo,Ephraim Kapungu. Picha na Elisa Shunda
Afisa
Mkuu wa Miradi wa Shirika lisilo la Kiserikali la British Council,
Atiya Sumar akizungumza katika ufungaji wa semina hiyo.
Meneja
Miradi wa Shirika Lisilo la Kiserikali la British Council, Ephraim
Kapungu (katikati) akielezea utendaji kazi wa shirika hilo katika
uwezeshaji wa masuala mbalimbali yahusuyo elimu jinsi shirika hilo
linavyofanya kazi zake kwa kushirikiana na serikali kupitia wizara ya
elimu.
Mmoja
kati ya wakufunzi wa semina hiyo Ndg.Edwin Shunda akiwa katika majukumu
yake ya ufundishaji na uwezeshaji wa uongozi kwa walimu wakuu wa shule
za msingi na sekondari wa Jiji la Dar es Salaam.
Washiriki wa Semina hiyo wakifuatilia mafunzo hayo kwa umakini mkubwa.
Afisa
Mkuu wa Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika kutoka Manispaa ya
Kinondoni,Saleh Hijja Mohamed (kushoto) akigawa cheti kwa mmoja wa
washiriki wa semina ya siku tatu ya mafunzo ya uongozi kwa walimu wa
shule za msingi na sekondari wa Jiji la Dar es Salaam leo. Semina hiyo
imefanyika katika Kituo cha Walimu cha Mzimuni kilichopo Magomeni
Mapipa. Kulia wanaoshuhudia ni Afisa Mkuu wa Miradi wa Shirika lisilo la
Kiserikali la British Council,Atiya Sumar na Meneja Miradi wa Shirika
hilo,Ephraim Kapungu. Picha na Elisa Shunda
Afisa
Elimu Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni,Kiduma Mageni akimpongeza mmoja wa
washiriki wa semina ya siku tatu ya mafunzo ya uongozi kwa walimu wa
shule za msingi na sekondari wa Jiji la Dar es Salaam leo.
Mgeni
rasmi, Afisa Mkuu wa Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika kutoka
Manispaa ya Kinondoni,Saleh Hijja Mohamed (katikati) akiwa na viongozi
wa shirika la British pamoja na walimu wakuu wa shule za msingi na
sekondari katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa semina ya siku
tatu ya mafunzo ya uongozi kwa walimu hao wa Jiji la Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment