Uongozi
mpya wa Shirikisho la Michezo la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI)
mara baada ya kutangazwa na msimamizi wa uchaguzi uliofanyika hivi
karibuni kwenye hoteli ya Mount Uluguru mkoani Morogoro.
SHIRIKISHO
la Michezo la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI), litatekeleza agizo
la Makamu wa Rais wa Tanzania Bara, Samia Suluhu Hassan kwa kuwa na
mabonanza kila mwisho wa mwezi yatakayohusisha wachezajiw a michezo
mbalimbali.
Moshi
Makuka, Katibu Mkuu wa SHIMIWI, alisema wamekubaliana katika kikao cha
kamati ya utendaji kilichofanyika hivi karibu, ambapo wataanza na
bonanza kubwa litakalofanyika Februari mwaka huu mkoani Dodoma, ambapo
sasa Wizara, Idara na Taasisi mbalimbali zimeshahamia mkoani hapo.
“Hili
bonanza litakuwa kubwa sana kwani ukiangalia tayari wizara, taasisi na
Idara za serikali kwa asilimia kubwa zimeshahamia Dodoma, hivyo timu
zianze kujiandaa na baada ya kukamilisha hili baadaye katika tarehe
zitakazotangazwa tutafanya tena Jijini Dar es Salaam,” alisema Makuka.
Makamu
wa Rais, mwaka jana alitoa agizo kufanyike mazoezi ya kila mwezi kwa
kuhusisha wafanyakazi ili kujijengea afya zao. Michezo inayochezwa
SHIMIWI ni pamoja na soka, netiboli, kuvuta kamba, baiskeli, karata, bao
na draft (wanawake na wanaume).
Mbali
na kuanza kwa mabonanza, pia Kamati hiyo ya Utendaji imeunda Kamati
mbalimbali ikiwemo ya Habari na Mawasiliano ambayo itaongozwa na Itika
Mwankenja (Mwenyekiti), Elias Malima (Katibu), huku wajumbe ni Bahati
Mollel, Jane John, James Katubuka, David Kitila na Jessey John; kamati
ya utendaji na nafasi zao ni Daniel Mwalusamba (Mwenyekiti), Ally
Katembo (Makamu Mwenyekiti), Makuka (Katibu Mkuu), Alex Temba (Katibu
Msaidizi), William Mkombozi (Mweka hazina), Frank Kibona (mweka hazina
msaidizi) na wajumbe ni Appolo Kayungi, Damian Manembe, Seleman Kifyoga,
Assumpta Mwilanga na Aloyce Ngonyani, huku wajumbe wa viti maalum ni
Mariam Kihange na Mwajuma Kisengo.
Wanaounda
Kamati ya Mipango ni Mwalusamba Mwenyekiti), Mkombozi (Katibu) na
wajumbe ni Makuka, Ngonyani, Kihange na John Jambele; huku kamati ya
Ufundi inaundwa na Kayungi (Mwenyekiti), Manembe (Katibu) na wajumbe ni
Kisengo na Joyce Benjamin; Kamati ya Nidhamu wapo Katembo (Mwenyekiti),
Temba (Katibu) na wajumbe ni Marcel Katemba na Mwilanga.
Kamati
ya usajili itaongozwa na Temba (Mwenyekiti), Kibona (Katibu) na James
Emmanuel (Mjumbe); nayo Sekretarieti ya Uendeshaji inaundwa na Kihange
(mwenyekiti), Kifyoga (Katibu), na wajumbe ni Bahati Magambo, Buya
Ndalija, Justo Mwandelile, Ahmed Chitagu, Peter Lihanjala, Gracia
Kyelula, Peter Onono, Modesta Kaunda, Amina Kakozi, Ismail Ismail,
Sophia Mkama na James Emmanuel.
Nayo
Kamati ya Huduma za tiba itaongozwa na Joakim Mwaipaja (Mwenyekiti),
Magreth Mtaki (Katibu), na Wajumbe ni Richard Yomba, Haji Masasi, Jafari
Chikoko na Gration Kaizirege.
No comments:
Post a Comment