Makamu Mkuu wa Chuo cha ATC anayeshughulikia Utawala,Fedha na Mipango,Dk Erick Mgaya akizungumza umuhimu wa shamba hilo ambalo litasaidia kuwapata wataalamu waliobobea nchini katika fani ya umwagiliaji.
Filbert Rweyemamu,Arusha
Balozi
wa Japan nchini,Masaharu Yoshida amesema serikali yake itaendelea
kusaidia sekta ya umwagiliaji nchini kwasababu ya umuhimu wake katika
kukuza uchumi na kuhakikisha usalama wa chakula.
Akizungumza
wakati wa kuweka jiwe la msingi la shamba la mafunzo Oljoro wilayani
Arumeru linalotumiwa na Chuo cha Ufundi Arusha(ATC) kwaajili ya mafunzo
ya vitendo kwa wanafunzi wanaosoma kozi ya Uandisi Umwagiliaji alisema
nchi yake ni mdau muhimu katika kuendeleza miradi ya umwagiliaji nchini.
"Mradi
huu ni alama muhimu ya urafiki wa nchi zetu katika kusukuma mbele
maendeleo ya kilimo ambacho kinachangia ajira kwa theluthi mbili na
kinatoa uhakika wa chakula,naamini wahitimu katika kozi watakua msaada
mkubwa kwa taifa hili,"alisema Yoshida
Balozi
Yoshida alisema nchi yake imekua ikizalisha kiasi kikubwa cha mpunga na
imewekeza kwenye miradi ya umwagiliaji zaidi 147 nchini kwa lengo la
kuinua uzalishaji wa zao hilo.
Kwa
upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha,Dk Masudi Senzia
alisema uendelezaji wa shamba la mafunzo Oljoro lenye ukubwa eka 150 ni
matokeo ya Chuo hicho kuanzisha mafunzo ya Umwagiliaji kupitia programu
yake ya Uandisi Ujenzi na Umwagiliaji katika ngazi ya Shahada.
"Maamuzi
ya kuanzisha programu hii yalikua na lengo la kuunga mkono dhana ya
serikali ya "Kilimo Kwanza" iliyokua na lengo la kupunguza uhaba wa
chakula nchini na katika kipindi hicho Chuo kilitambua upungufu wa
wataalamu,"alisema Dk Senzia
Alisema
baada ya kupata wataalamu wawili kutoka shirika la kimataifa la
maendeleo la Japan(JICA) mwaka 2011 Hiroshi Mizumi na Takashi Katsumi
Chuo kiliongezewa nguvu na kuanza utekelezaji wake.
Dk
Senzia alisema mwaka 2010 walioanza kozi ya Uandisi Ujenzi na
Umwagiliaji walipata wanafunzi 25 lakini walioanza masomo mwaka huu ni
205 kati yao mafundi Sanifu ni 60 na Waandisi 145 na kwamba hadi kufikia
mwaka 2017 wahandisi 100 wameshahitimu na kutunukiwa Shahada zao.
Mtaalamu
wa Umwagiliaji kutoka JICA,Naoyuki Matsuoka alisema mradi huo wa miaka
minne unaofikia kikomo mwezi Machi mwaka huu alisema shirika lake
limetoa kiasi cha zaidi ya Sh 3 bilioni kufanikisha mradi huo.
|
No comments:
Post a Comment