Pages

January 27, 2018

RAIS MSTAAFU KIKWETE AFURAHIA SOMO LA MKIKITA KUHUSU KILIMO BORA CHA PAPAI

 Rais mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete akifurahi kuona papai alililopelekewa na Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita/Livinggreen) walipokwenda kumpa elimu kuhusu kilimo bora cha zao hilo nyumbani kwake Msoga, Chalinze mkoani Pwani. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange.
 Dk. Kikwete akishukuru kwa mafunzo hayo yaliyotolewa na Mwanachama wa Mkikita  Mtaalamu wa Kilimo cha Papai kutoka Kampuni ya Awino Farm, Ezra Machogu. Kulia ni Adam NGAMANGE


Na Richard Mwaikenda, Msoga.

.RAIS mstaafu Dk.Jakaya Kikwete amefurahishwa na elimu ya kilimo cha kisasa cha Papai chenye gharama nafuu aliyopatiwa na Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita/Living green)

Elimu hiyo ilitolewa hivi karibuni nyumbani  kwake Msoga, Chalinze, mkoani Pwani na Ezra Machogu  Mtaalamu wa Kilimo wa Kampuni ya Awino Farm ambayo ni mwanachama wa Mkikita.

Kikwete alifurahi kuambiwa kwamba kampuni hiyo inaweza kuzalisha papai lenye ubora kwa kutumia teknolojia ya kisasa yenye gharama nafuu hivyo kumfanya mkulima apate faida kubwa wakati wa mauzo.

Ezra anasema kuwa unaweza kupunguza gharama kwa kuacha kuchimba mashimo badala yake unalima shamba mara tatu kwa kutumia trekta, hivyo kuufanya udongo kuwa tifutifu kitendo kitakacho kurahisishia kupanda miche ya papai bila matatizo.

Anasema ukitumia njia hiyo itakuondolea gharama ya kuchimba mashimo 1200 katika heka moja ambayo jumla ni sh. mil. 6 ikiwa kila shimo itakuwa sh. 500 wakati kulima mara tatu heka moja kwa trekta ni sh. 150,000.

Ezra anamweleza Dk. Kikwete kuwa unaweza pia kupunguza gharama ya mbolea kwa kila shimo kuweka majagi mawili badala ya debe moja.Pia alimweleza kuwa katika umwagiliaji papai halihitaji maji mengi, hivyo unaweza kutumia lita 10,000 kwa siku kumi badala ya siku nne.

Alisema kuwa pia wamejipanga kimasoko kwa kuutumia mtandao wa Mkikita ambao tayari una watalaam wa masoko ya ndani na nje ya nchi pamoja na watalaamu wa kufungasha (Packaging) bidhaa kwa teknolojia ya kisasa.

Baada ya kuridhika na maelezo hayo, Rais mstaafu, alifurahi na kuishukuru Mkikita kwa kumpelekea watalaam hao kutoka Kampuni ya Awino Farm.Ezra alizidi kumfurahisha, Dk. Kikwete kuwa kwa heka moja akiuza papai anaweza kupata hadi sh. mil. 80,000,000 kwa mchanganuo ufuatao; 

Heka moja inaweza kupandwa mipapai 1000 hadi 1200 na kwamba mpapai mmoja unaweza kuzaa papai 100 hadi 1300 na endapo kila papai lenye uzito wa kilo 2 likiuzwa kwa bei ya jumla sh. 800 ukizidisha na wastani wa papai 100 kila mche halafu zidisha kwa miche 1000 tu unapata kiasi hicho cha fedha kwa msimu wa kwanza.

Pia alimueleza kuwa uzuri wa miche ya papai huishi miaka mitatu ambapo kila wiki utakuwa unavuna na kuuza, hivyo kukupatia faida kubwa tofauti na mazao mengine ambayo ukivuna mara moja tu.

"Laiti kama ungekuwa mchungaji, padri au sheikh anayehubiri kutafuta waumini, basi bila shaka mimi mmenipata nimekuwa muumini wenu." Alisema Dk. Kikwete huku akicheka kwa furaha."Kubwa mlilonifurahisha ni jinsi mlivyopunguza kwa kiasi kikubwa gharama ya kuzalisha papai 
na faida kubwa nitakayoipata, nipo tayari kutoa heka 10 za kuanzia."Aliahidi Dk. Kikwete ambaye alisema kazi ya kilimo anaipenda na kwamba iko kwenye damu yake. 

Ujumbe huo uliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita Adam Ngamange, ambaye akabla y yote alimshukuru Dk. Kikwete kwa kuwaalika na kumuomba ajiunge na mtandao, jambo ambalo alilikubali.

Ujumbe alioongozana nao ni Ezra Machogu, Martine  Wamaya wa Kampuni ya Awino Farm, Khalid Tamim, Hassan Tamim na Ali Said ambao ni Wawekezaji wa zao la muhogo,  Mkurugenzi  Betl Worldwide Ltd, Murtaza Bharmal ambaye ni mtaalamu wa masoko na uongezaji thamani mazao na Richard Mwaikenda ambaye ni Mshauri wa Habari wa mtandao huo.
 Meneja  Kilimo wa Mashamba ya Dk. Kikwete, Justine (kushoto) akiwa na  Mkurugenzi wa Kampuni ya Awino, Martine Wamaya (kulia) na Mtalaamu wa kilimo cha Papai,  Ezra Machogu walipokuwa wakitoka kuchuma papai kutoka kwenye shamba darasa la Kampuni ya Awino eneo la Msata tayari kumpelekea Rais mstaafu, Dk. Kikwete. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Dk. Kikwete akisalimiana na Adam Ngamange wa Mkikita
 Dk. Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa Awino Farm, Wamaya.
 Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mtaalamu wa Kilimo cha Papai, Ezra
 Dk. Kikwete akisalimiana na wanachama wa Mkikita wawekezaji katika shamba la Muhogo. Kushoto ni Khalid Tamim na Hassan Tamim.
 Meneja wa Kilimo wa Mashamba ya Dk. Kikiwete, Justine akiutambulisha ujumbe wa Mkikita nyumbani kwa Kikwete, Msoga
 Ngamange akielezea mbele ya Dk Kikwete kuhusu utendaji wa mtandao huo
 Mtaalamu wa Kilimo cha Papai, Ezra (kulia) akitoa elimu kwa Dk. Kikwete kuhusu kilimo bora cha zao hilo kwa gharama nafuu
 Ngamange akimkabihi Dk. Kikwete mafuta yaliyotengenezwa kwa kutumia mchaichai
 Dk. JK akinusa mafuta hayo ya mchaichai

 Dk. Kikwete akifungua kasha la mchaichai
 Mtaalamu wa Masoko na Ufungashaji wa bidhaa mshirika wa Mkikita, Murtaza Bharmal (kulia) akitoa maelezo jinsi anavyoweza kutafuta masoko kirahisi kwa kutengeneza makasha mazuri ya kuhifadhia bidhaa ili kuongeza thamani.
 J akiwa na ujumbe wa Mkikita pamoja maofisa wasaidizi wake
 Dk. Kikiwete akizungumza Ngamange (kulia) pamona na Murtaza
 JK akiagana na kiongozi wa ujumbe wa Mkikita, Ngamange baada ya ziara yao kumalizika

JK akiagana na mwandishi wa habari wa Azam TV, Octor

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...