*Philison Mdee aongoza kwa wavulana, Ellizabeth Mangu aongoza wasichana
*Wengine 265 matokeo yafutwa, yumo aliyeandika matusi kwenye majibu
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
SHULE
ya Sekondari ya St.Francis Girls imeongoza kwa kushika nafasi ya kwanza
kitaifa katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2017.
Akitangaza
sekondari ambazo zimeshika nafasi za juu kwenye matokeo hayo, leo
jijijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk.Charles Msonde
amesema nafasi ya pili imechukuliwa na sekondari ya Feza Boys na nafasi
ya tatu sekondari ya Kemebos.
Wakati
nafasi ya nne imeshikiliwa na sekondari ya Bethel Saabs Girls, nafasi
ya tano sekondari ya Anuarite, nafasi ya sita sekondari ya Marian Gilrs
huku nafasi ya saba ikishikiliwa na sekondari ya Canossa, wakati nafasi
ya nane imechukuliwa na sekondari ya Feza Girls, nafasi ya tisa
sekondari ya Marian Boys na nafasi ya 10 sekondari ya Shamsiye Boys
WALIOONGOZA 10 BORA KITAIFA
Kwa
upande wa wanafunzi ambao wameshika nafasi ya kwanza hadi ya kumi
kitaifa kwenye matokeo hayo, Dk.Msonde alisema nafasi ya kwanza
imeshikwa na mwanafunzi Philison Mdee(Marian Boys), wakati nafasi ya
pili imeshikwa na Eliza Mangu(Marian Girls), nafasi ya tatu
Ana Mshana(Marian Girls)
Ametaja
nafasi ya nne imeshikwa na Emanuel Makoye(Ilboru), nafasi ya tano
Lukelo Luoga(Ilboru), nafasi ya sita Fuad Thabit(Feza Boys), nafasi ya
saba Godfrey Mwakatage(Uwata), nafasi ya nane Baraka Mohamed(Angeles),
nafasi ya tisa Lilian Moses(Marian Girls) na nafasi ya kumi kitaifa
imechukuliwa na Everine Mlowe(St. Francis Gr)
WAVULANA 10 BORA KITAIFA
Akitangaza
walioshika nafasi ya kwanza hadi ya 10 kitaifa kwa mujibu wa Dk.Msonde
ni Philison Mdee(Marian Boys), nafasi ya pili Lameck Makoye(Ilboru),
nafasi ya tatu Tadei Luoga(Ilboru), nafasi ya nne Fuad Thabit (Feza
Boys).
Wakati
nafasi ya tano ni Godfrey Mwakatage(Uwata),nafasi ya sita Baraka
Mohamed(Angeles),nafasi ya saba Noel Shimba(Marian Boys), nafasi ya
nane ni Patrick Robert(Mzumbe), nafasi ya tisa Robison Eliona(ILboru) na
nafasi ya 10 bora kitaifa imechukuliwa na mwanafunzi Harrison Simkoko
(Mzumbe)
WASICHANA 10 BORA KITAIFA
Dk.Msonde
ametaja wasichana walioongoza kwenye matokeo ya mtihani huo ambapo
nafasi ya kwanza imechukuliwa na Ellizabeth Mangu(Marian Girls) nafasi
ya pili Anna Benjamin Mshana(Marian Girls), watatu ni Lilian Moses
Katabalo(Marian Girls) na nafasi ya nne ni Eveline Edward
Mloe(St.Francis Girls).
Nafasi
ya tano imechukuliwa na Rosemary Godfrey Ritth (St.Francis), nafasi ya
sita ni Priscilla Hermenegild Kiyagi(St.Francis) nafasi ya saba ni
Comfort Aloyce Mkangaa (St.Francis), nafasi ya nane Reginelly Gaudence
Moshi(Kifungilo Girls) nafasi ya tisa Maria Hewa Gambaloya(Mariam Girls)
na nafasi ya 10 ni Dorice Humphrey Shadrack(St.Francic)
UFAULU WAONGEZEKA KWA ASILIMIA SABA
Akizungumzia
matokeo hayo, Dk.Msonde amefafanua kuwa ufaulu umeogezeka kwa asilimia
saba na kwamba jumla ya watahiniwa 385, 767 walisailiwa kufanya mtihani
kidato cha nne mwaka 2017.
Ameongeza
kati yao watahiniwa 287,713 sawa na asilimia 77.09 wamefaulu na kati
yao wasichana ni 143,728 sawa na asilimia 75.21 na wavulana ni 143,985
sawa na asilimia 79.06.
"Mwaka
2016 watahiniwa waliofaulu walikuwa 277,283 sawa na asilimia
70.09.Matokeo ya watahiniwa 50 wa shule waliopata matatizo ya kiafya na
kushindwa kufanya baadhi ya masomo ya mitihani hiyo, watapata fursa hiyo
mwaka huu,"amesema Dk.Msonde.
Ameeleza
pia NECTA imeamua kufuta matokeo ya watahiniwa 265 ambao wamebainika
kufanya udanganyifu wakati wakifanya mtihani huo."Kuna mmoja ya mtihani
tumekuta mtahiniwa ameandika matusi kwenye haratasi ya majibu,"amesema
Dk.Msonde.
No comments:
Post a Comment