Balozi
wa Tanzania Nchini Malawi, Balozi Benedicto Mashiba kushoto,
akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Nkhata Bay nchini Malawi Alex Mdooa
mara baada ya meli kuwasili bandarini hapo
Mkuu
wa bandari za Ziwa Nyasa, Ajuaye Msese kushoto, akitoa maelezo kwa
Balozi wa Tanzania Nchini Malawi, Balozi Benedicto Mashiba kulia,
katikati kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nkhata Bay nchini Malawi Alex
Mdooa
MV Njombe ilipowasili bandari ya Nkhata Bay nchini Malawi
MV Njombe mara baada ya kutia nanga bandari ya Nkhata Bay nchini Malawi
Kuanza
safari kwa Meli za kisasa za mizigo za MV Njombe na MV Ruvuma ambazo
zina uwezo wa kubeba uzito wa tani 1,000 kumefungua fursa za kibiashara
kati ya Tanzania, Malawi na Msumbiji.
Meli
ya Mv Njombe ambayo imefanya safari yake kwa mara ya kwanza nchini
Malawi imefika salama na kutia nanga katika bandari za Nkhata Bay. Meli
ya Mv Ruvuma inayopakia shehena ya Clinker inatarajiwa kutia nanga
katika Bandari ya Monkey Bay nchini Malawi siku mbili zijazo.MV
Njombe ambayo ilibeba takribani tani 800 ya shehena ya saruji kutoka
bandari ya Kiwira nchini Tanzania hadi bandari ya Nkhata Bay nchini
Malawi imetia nanga salama na imetumia muda mfupi zaidi kufika Malawi.
MV
Ruvuma ambayo ni pacha wa MV Njombe nayo imepakia takribani tani 800 za
shehena ya ‘Clinker’ katika bandari ya Kiwira nchini Tanzania kuelekea
bandari ya Monkey bay nchini Malawi.Akizungumzia
ujio wa shehena hizo za Saruji na ‘Clinker’, Balozi wa Tanzania nchini
Malawi ambaye pia alikuja kushuhudia tukio hilo, Mheshimiwa Benedicto
Mashiba amesema kwamba kuanza kwa safari hizo ni habari njema kwa
wafanyabiashara wa Tanzania na Malawi .
Balozi
Mashiba amesema kwamba, ujio wa meli hizo ni ufunguo wa biashara kati
ya Tanzania na Malawi kwani kusafirisha bidhaa kwa njia ya maji ni nafuu
na salama zaidi ukilinganisha na barabara.
“Usafiri
huu ni mkombozi kwa wananchi na wafanyabiashara wa nchi hizi mbili
(Malawi na Tanzania) kwani utawezesha usafirishaji wa mizigo kwa wingi
ukilinganisha na njia nyingine kama barabara,” amesema Balozi Mashiba.Mashiba
amesema kwamba kuna biashara kubwa ya kusafirisha mizigo kati ya
Tanzania, Malawi na Msumbiji kupitia Ziwa Nyasa hivyo kuanza safari kwa
meli hizo kutasaidia kuongeza zaidi ukubwa wa shehena katika ya nchi
hizo.
Naye
Mkuu wa bandari za Ziwa Nyasa, Bw. Ajuaye Msese amewasihi wananchi na
wafanyabiashara wa Tanzania, Malawi na Msumbiji kutumia usafiri huo
kwani ni wa uhakika, nafuu na salama.Msese
amesema kwamba kusafirisha shehena ya bidhaa kama ‘Clinker’, saruji na
makaa ya mawe pamoja na bidhaa nyingine kwa wingi ni salama zaidi
ukitumia njia ya maji kuliko barabara.
Amesema
mbali na hilo na usalama na unafuu, lakini pia tukisafirisha bidhaa kwa
kutumia maji tunaokoa uharibifu wa miundombinu yetu kama barabara na
madaraja.Mkuu
huyo wa bandari za Ziwa Nyasa alitolea mfano mzigo wa saruji ulioletwa
na meli ya MV Njombe pekee, kama ungekuja kwa njia ya barabara, basi
msafirishaji angelazimika kutumia malori 25.
“Ukisafirisha
mzigo kwa njia ya maji ni nafuu, salama na unakuwezesha kusafirisha
mzigo mkubwa zaidi kwa wakati mmoja,” amesema Msese.Kwa
mujibu wa Bw. Msese, ukisafirisha mzigo kwa njia ya maji na kwa wingi
kama huu, itamsaidia mlaji wa mwisho kuja kupata bidhaa hizo kwa bei
nafuu.
Ziwa
Nyasa ni moja kati ya maziwa makuu yanayounganisha mikoa ya Mbeya,
Ruvuma na Songea na nchi za Malawi na Msumbiji kwa njia ya maji.
No comments:
Post a Comment