Mkurugenzi
Mtendaji wa Kiwanda cha Sunflag cha mjini Arusha, Ajay Shah, akiongoza
zoezi la kuchoma nyavu haramu za dagaa zilizo chini ya sentimita 8
(marobota 584) zenye jumla ya shilingi milioni mia moja zilizokamatwa
kwenye Kiwanda chake na Kikosi Kazi Maalum cha Kutokomeza Uvuvi Haramu
nchini kilichoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Joelson
Mpina kwenye dampo la takataka nje kidogo ya jiji la Arusha.(Na John
Mapepele)
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Joelson Mpina (mwenye kofia) akikagua
chumba cha baridi cha kuhifadhia samaki (Cold room) cha kampuni ya Alpha
Choice mjini Arusha akiwa katika operesheni maalumu ya kudhibiti
uvuvi haramu kulia ni mmliki wa kampuni hiyo Yussuf Khatry.
Marobota
584 ya nyavu haramu yaliyotengenezwa na Kiwanda cha Sunflag cha mjini
Arusha yenye thamani ya shilingi milioni 100 wakitekea kwenye dampo nje
ya jiji la Arusha . Marobota hayo alikamatwa na Kikosi Kazi Maalum
cha Kutokomeza Uvuvi Haramu nchini kilichoundwa na Waziri wa Mifugo na
Uvuvi, Mhe. Luhaga Joelson Mpina ambapo uteketezaji huo uliongozwa na
mmliki wa kiwanda hicho Ajey Shah.
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Joelson Mpina (mwenye kofia)
akisikiliza taarifa ya ukamataji wa marobota 584 ya nyavu haramu
yaliyotengenezwa na Kiwanda cha Sunflag cha mjini Arusha yenye thamani
ya shilingi milioni 100 kutoka kwa kiongozi wa Kikosi Kazi Maalum cha
Kutokomeza Uvuvi Haramu nchini West Mbembati aliye kulia, kushoto
mwakilishi wa Afisa Tawala wa Mkoa wa Arusha David Lyamongi.
Na John Mapepele
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina amekitoza faini ya Shilingi
milioni mia moja Kiwanda cha Sunflag Tanzania Limited cha jijini Arusha
baada ya kukutwa na makosa mawili ambayo ni kuzalisha na kuuza nyavu
bila kuwa na leseni kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kuzalisha na
kuuza nyavu ambazo ziko kinyume na matakwa ya Sheria ya Uvuvi namba 22
ya mwaka 2009.
Kulingana
na maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Ajay Shah, kiwanda
kimekuwa kikitengeneza vyavu hizo haramu kwa miaka mitatu mfululizo sasa
ambapo inakadiliwa kuwa tayari kimeshatengeneza tani 1296 nyavu hizo
zenye thamani ya shilingi bilioni nne.
Akitoa
taarifa kwa Waziri Mpina, Kiongozi wa kikosi kazi cha kutokomeza uvuvi
haramu katika kanda ya Ziwa Victoria, West Mbembati amesema kuwa tarehe
17/1/2018 walifika kwenye kiwanda hicho na kukamata marobota 584 yenye
thamani ya milioni mia kufuatia maelekezo ya Waziri Mpina yaliyotolewa
Mjini mwanza hivi karibuni baada ya mfanyabiashara Dastan Venanti
kukamatwa na nyavu hizo zenye thamani ya milioni sitini na tano ambazo
nyaraka zilionyesha alinunua katika kiwanda hicho.
Akipokea
taarifa hiyo Waziri Mpina alisema mkakati uliopo kwa sasa ni kuwabaini
watengenezaji na wasambazaji wote wa zana haribifu za uvuvi ikiwa ni
pamoja na vyavu zisizoruhusiwa kisheria ambapo amesema hatua za kali za
kisheria dhidi yao zitatumika ili kudhibiti uvuvi haramu kwenye
maji(mito,maziwa na bahari) ya nchi yetu.
“Operesheni
ya kuwabaini na kuwachukulia hatua wafanya biashara wakuu wanaofadhili
na kuendeleza biashara ya uvuvi haramu ni ya kudumu ambapo mkakati
uliopo sasa ni kuwanyang’anya na kuwafutia lesseni zao za biashara”
alisisitiza Mpina
Aliwaonya
wafanyabiashara wanaosafirisha samaki na mazao yake katika nchi za
jirani za Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kongo wanaotishia kugoma
ambapo amesisitiza kwamba hatua waliyoichukuwa ni ndogo badala yake
waachane kabisa na biashara hiyo kwa kuwa wamekuwa wakikwepa kodi na
kuikosesha Serikali mapato yake kwa muda mrefu.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho, Ajay Shah alikiri
kutenda makosa hayo na kueleza kuwa kiwanda kimekuwa kikiendelea
kutengeneza vyavu hizo bila kujua kuwa kilikuwa hakizingatii sheria za
Uvuvi ambapo alisema kimekuwa kinauza nje ya nchi hususan kwenye soko la
Nairobi nchini Kenya na Mwanza
Aliwataja
baadhi ya wateja wake wakuu wa mkoani Mwanza kuwa ni pamoja na Dastan
Venant, Morice Otieno na Majani Masagati ambao wote walikamatwa hivi
karibuni na nyavu zisizoruhusiwa kisheria na kikosi kazi cha kudhibiti
uvuvi haramu kilichoundwa na Waziri Mpina na kutozwa faini ya jumla ya
shilingi milioni 120 huku vyavu hizo zikitaifishwa na kuteketezwa mara
moja.
Katika
hatua nyingine Mkurugenzi huyo aliongoza zoezi la kuteketeza nyavu hizo
haramu kwa kushirikiana na Waziri na Watendaji mbalimbali wa Serikali
katika dampo la kuwekea takataka nje kidogo ya jiji la Arusha huku
akikiri kuwa atazingatia taratibu zote za Serikali katika kutengeneza
nyavu zinazoruhusiwa kisheria ambapo alisema tayari wameshapeleka barua
Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kupata kibali cha kutengeneza nyavu.
Aidha
Waziri Mpina ametoa siku tatu kwa Watendaji wa Wizara yake kumempatia
kibali cha kutengeneza nyavu hizo kwa mujibu wa sheria za nchi.
Kulingana na Sheria ya Uvuvi namba 22 ya Mwaka 2003 kibali hicho
kinatolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi.
No comments:
Post a Comment