Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Mohamed Shein
amefungua Soko Jipya la Kinyasini lililojengwa na Programu ya Miundo
Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini
(MIVARF) ili kutatua changamoto za kukosekana kwa soko la kisasa katika
Mkoa wa Kaskazini litakalowasaidia wafanyabiashara wadogo wadogo
kuendesha biashara zao.
Mhe.
Rais Shein amesema soko hilo litawagusa na kuwafikia watu wenye kipato
cha chini kuinuka kiuchumi kwa kuwanufaisha Wajasiliamali wadogo
wadogo vijijini pamoja na wafanyabiashara; Asasi ndogo ndogo za kifedha
zinazotoa huduma vijijini; Vyama vya Msingi vya Ushirika/ Asasi za
vijijini zinazojishughulisha na usindikaji wa mazao na masoko ya mazao
kwa kushirikisha wanawake katika makundi yote.
Katika
uzinduzi huo uliofanyika Januari 09, 2018 Mkoa wa Kaskazini katika eneo
la Kinyasini, Mhe.Rais alisema kujengwa kwa soko hilo kuna manufaa
makubwa kwa wakulima wadogo wakiwemo wafugaji, wavuvi na wafanya kazi za
mikono.
“Soko
hili litakuwa lenye tija kubwa kwa wananchi wa Zanzibar bila kujali
maeneo wanakotoka. Soko hili ni letu sote, lisingeweza kujengwa kila
mahali, au hewani lazima lingewekwa mahali, hivyo eneo hili la Kaskazini
lilipata fursa hii, hivyo niwaombe liwe la wananchi wote wa
Zanzibar.”Alisema Mhe.Rais
Sambamba
na hilo Mhe. Rais alieleza kuwa kujengwa kwa soko hilo ni moja ya
matunda ya Muungano na kuwataka Wananchi kuuenzi na Kuulinda Muungano
huo.
“Miradi
hii inayohusisha Bara ni moja ya mafanikio na matokeo makubwa ya
Muungano wetu na hatuna budi kuuenzi”Alisisitiza Dkt.Shein
Katika
hatua nyingine,Mhe. Rais aliitaka Halmashauri husika kuendelea kuweka
mikakati mizuri ya kulitunza na kuliendeleza ili liweze kuleta tija
iliyokusudiwa kwa Wazanzibar wote.
“Niwaombe
Halmashauri Kuona njia nzuri za kuendeleza kazi hii iliyofanywa na
Programu hii na kuhakikisha wananchi wananufaika zaidi kama
ilivyokusudiwa”Alisisitiza Mhe.Rais
Kwa
Upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala
ya Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.
Jenista Mhagama aliwataka wananchi kuunga mkono jitihada za Serikali kwa
kuzingatia mafanikio ya mradi huu ikiwemo kusaidia kupambana na
umasikini na kuleta tija.
“Kuwepo
kwa soko hili kutasaidia kupambana na umasikini na kuongeza mapato,
hivyo washiriki watunze miundombinu hiyo pamoja na kuongeza thamani ili
kuleta tija.”Alieleza Mhe.Mhagama .
Naye
Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar Mhe.Hamad Rashid Mohamed alimalizia kwa kuishukuru Ofisi ya
Waziri Mkuu kupitia Programu ya MIVARF kuona umuhimu kuwajengea soko
lenye ubora na litakalo tatua changamoto za kukosa soko la uhakika.
“Soko
hili la Kinyasini moja kati ya masoko 16 yaliyojengwa na Programu hii
katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hivyo litasaidia kuondokana na
umasikini na wananchi kujikwamua kiuchumi”
Programu
hii ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha
Vijijini (MIVARF) inatekelezwa katika Halmashauri 62 za Tanzania Bara na
Wilaya 10 za Zanzibar, ikiwa imegharamiwa na Benki ya Maendeleo ya
Afrika, Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo, Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kwa kusimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na Kushirikiana na
Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo, na Uvuvi Zanzibar.Programu ilianza
utekelezaji wake Mwaka 2012.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Ali Mohamed
Shein akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Soko jipya la Kinyasini
lililojengwa na Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na
Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu
Januari 09, 2018 eneo la Kaskazin ‘A’ Zanzibar.Kulia ni Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu),
Mhe.Jenista Mhagama na kushoto kwake ni Waziri wa Kilimo,Maliasili,
Mifugo na Uvuvi Mhe. Hamad Rashid Mohamed.
Mhandisi
wa Kampuni ya ZECCON Bw.Ali Mbarouk Juma akitoa maelezo ya kitaalamu
kuhusu ujenzi wa Soko la kinyasini kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Ali Mohamed Shein wakati wa uzinduzi wa
Soko hilo lililojengwa eneo la Kaskazin ‘A’ Unguja, Zanzibar.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Ali Mohamed
Shein akihutubia Wananchi waliohudhuria katika uzinduzi wa Soko la
Kinyasini lililojengwa na Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji
Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) chini ya Ofisi ya Waziri
Mkuu.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu)
Mhe.Jenista Mhagama akitoa maelezo mafupi ya Soko la Kinyasini wakati
wa uzinduzi wa Soko hilo Januari 09, 2018 Lililojengwa katika mkoa wa
Kaskazin ‘A’ Unguja
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Ali Mohamed
Shein akimpa mkono wa pongezi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama mara baada ya
kuwasilisha maelezo mafupi kuhusu soko la Kinyasini lililozindulia
Januari 09, 2018.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Ali Mohamed
Shein akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Serikali
pamoja na Viongozi wa Soko jipya la Kinyasini mara baada ya Uzinduzi
Januari 09, 2018. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
No comments:
Post a Comment