Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WAZIRI
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dk.Augustine Mahiga
amesema kuwa ili kufikia uchumi wa viwanda ni muhimu kutengeneza
mazingira mazuri ya kuwavutia wawekezaji katika sekta mbalimbali
zikiwamo za sheria, kodi, ajira,vvivutio vya uwekezaji na kilimo.
Dk.Mahiga,
ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na
waandishi wa habari baada ya kumaliza kuzindua kongamano la siku mbili
lililoandaliwa na Ubalozi wa India nchini Tanzania kwa kushirikisha nchi
wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na Jumuiya ya
Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
Lengo
la kongamano hilo pamoja na mambo mengine washiriki wamezungumzia namna
ya ushiriki wa sasa na siku zijazo unavyoweza kuleta amani katika nchi
wanachama wa jumuiya hizo.Kauli mbiu ya kongamano katika kongamano hilo
inasema "Amani, utulivu na maendeleo".
Dk.
Mahiga amefafanua jambo hilo si jipya kuzungumzwa isipokuwa bado
halijaeleweka na hivyo linatakiwa kuzunguzwa Tanzania pamoja EAC.
“Tunamkakati
madhubuti wa kujenga viwanda katika EAC na SADC. Sasa kusema nataka
viwanda ni kingine, kuvuta viwanda ni kingine, kufanya viwanda vizalishe
na vistawi ni jambo lingine.
"Na
ukisema unataka viwanda mazingira yapo? unataka kufanikisha viwanda
je utaalam upo? hapo sasa kupitia mambo hayo matatu unaweza kuendesha
viwanda,” amesema Dk.Mahiga.
Ameongeza
katika kongamano hilo watazungumzia kinadharia kuhusu amani na jumuiaya
hizo zinavyochagia kuleta amani katika nchi na namna mchanganyiko wa
amani unavyoweza kuleta maendeleo katika mataifa hayo yanayoshirikiana.
Amewakumbusha
washiriki wa kongamano hilo kuwa "Hapa tumekumbuka mchango wa
mwanaharakati mkubwa Mahatma Ghandhi aliyeliyesisimua dunia kutokana na
mapambano yake na Waingereza ili kuleta uhuru wa wa India na viongozi
wengi wa Afrika waliiga mfano huo na hata Hayati Mwalimu Jualias Nyerere
aliwahi kusema kuwa alijifunza kutoka kwake.
Pia
Dk. Mahiga amesema nchi ya India ni kubwa na ina watu zaidi ya
Sh.bilioni 1.2 na wana amani na wamekuwa wakifanya uchaguzi kwa
demokrasia na kubwa zaidi wamejiimarisha kiuchumi na kuwa miongoni mwa
nchi ambazo uchumi wake upo imara na kueleza ipo haja kwa nchi nyingine
kuiga kutoka Taifa hilo.
"Amani
inaweza kutazamiwa ndani ya nchi kama unatengeneza taasisi za
ushirikishi na uwajibikaji na si tu kudumisha amani bali kuleta utulivu
wa kisiasa,"amesema Dk.Mahiga.
Naye
aliyewahi kuwa Balozi wa Kwanza nchini India mwaka 1994 na Waziri Mkuu
Mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, amesifu uhusiano wa kidiplomasia uliopo
kati ya Tanzania na India na hayo ni matunda ya Hayati Mwalimu Nyerere
na Waziri Mkuu wa kwanza wa India Jawaharial Nehru.
Kwa
upande wa Balozi wa India nchini, Sandeep Arya, amesema pamoja na
kujadili masuala ya ushirikiano Serikali ya India itatumia fursa ya
kongamano hilo kukusanya maoni, mapendekezo na taarifa ambayo yatatolewa
na washiriki waliopo na pamoja na wadau hasa wamasuala ya ulinzi, amani
na maendeleo ili kila Taifa lifikie malengo ya kitaifa na kuboresha
maisha ya wananchi wake.
Ameelezea
namna ambavyo India imekuwa ikishirikiana na nchi zilizopo Bara la
Afrika ikiwamo Tanzania katika kufanikisha upatikanaji wa maendeleo
kwenye nyanja mbalimbali.
Waziri
Mkuu Mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim akizungumza leo jijini Dar es
Salaam kwenye Kongamano la siku mbili lililoandaliwa na Ubalozi wa India
nchini Tanzania kwa kushirikisha nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC) pamoja na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa
Afrika (SADC).
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dk.Augustine Mahiga
akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua rasmi Kongamano
la siku mbili ambalo limeandaliwa na Ubalozi wa India nchini
Tanzania.Kauli mbiu ya kongamano hilo ni Amani, Utulivu na Maendeleo.
No comments:
Post a Comment