Baadhi
ya wanachama wa CCM waliohudhuria mkutano wa uzinduzi wa kampeni za
uchaguzi mdogo wa jimbo la Singida kaskazini wakiwa kwenye viwanja vya
mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Mtinko,singida vijijini juzi.
Baadhi
ya wanachama wa CCM waliohudhuria mkutano wa uzinduzi wa kampeni za
uchaguzi mdogo wa jimbo la Singida kaskazini wakiwa kwenye viwanja vya
mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Mtinko,singida vijijini juzi.
Naibu
katibu Mkuu wa CCM Tanzania bara,Rodrick Mpogolo akizindua kampeni za
uchaguzi mdogo wa CCM katika jimbo la Singida kaskazini zilizofanyika
juzi katika Kijiji cha Mtinko,singida vijijini.
Mgombea
wa kiti cha ubunge wa jimbo la Singida kaskazini,Justine Monko akiwa
tayari amepokea ilani ya chama kwa ajili ya kutekeleza yaliyoainishwa
ndani ya ilani hiyo.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)
Na,Jumbe Ismailly SINGIDA
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida kimezindua kampeni zake za uchaguzi
mdogo katika jimbo la Singida Kaskazini na kusisitiza juu ya kudumisha
amani,utulivu na mshikamano uliopo hapa nchini.
Akizindua
kampeni hizo zilizofanyika katika Kijiji cha Mtinko,Singida
Vijijini,kwa niaba ya Katibu mkuu wa CCM taifa,Naibu katibu mkuu wa
CCM,Tanzania bara,Rodrick Mpogolo alisema idadi kubwa ya wananchi
wameendelea kukichagua chama cha mapinduzi kutokana na kuwa na mipango
mizuri ya maendeleo.
Alizitaja
sababu zingine kuwa ni chama chenye historian a pia kina awamu tano za
uongozi na kwamba ni chama kilichokomaa na endapo kitakabidhiwa nchi au
ukikabidhi madaraka,watakuwa na uhakika kwamba madaraka hayo yameshikwa
na watu waliokomaa.
Kwa
mujibu wa Naibu katibu mkuu huyo wakati wote CCM imekuwa ikishughulikia
kero za watu na kwa hivi sasa inayo matumaini makubwa ya kubadilisha
maendeleo ya nchi na kwamba hivi sasa rais wan chi amekwisha hamisha
makao makuu ya serikali yake Mkoani Dodoma,jirani kabisa na Mkoa wa
Singida.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dk.Rehema Nchimbi pamoja na
kuwashawishi wananchi wa jimbo la Singida kaskazini kumchagua mgombe wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) lakini hakusita pia kutaja utekelezaji
unaofanya na serikali ya chama hicho kwa hivi sasa.
Dk.Nchimbi
ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa Mkoa wa
Singida aliweka bayana kwamba mradi wa usambazaji umeme vijijini awamu
ya pili nay a tatu umeshaanza na tayari zaidi ya shilingi bilioni 71.3
zinatarajiwa kutumika kusambaza nishati hiyo katika vijiji vyote.
“Kwa
hivyo nawaombeni wananchi wa jimbo la Singida kaskazini mchagueni
mgombea wa CCM kwani mkimleta mtu mwingine haijui ataanza kwanza
kujifunzafunza atatuchelewesha,kwa hiyo mleteni Monko ili aendeleze
utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)”alisisitiza Dk.Nchimbi.
Akimkaribisha
Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida,Juma Hassani
Kilimba alisema kutokana na wingi wa wananchi waliohudhuria mkutano huo
wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo,unadhihirisha wazi kwamba wao
tayari kumchagua mgombea huyo wa CCM ifikapo jan,13,mwaka ujao.
Hata
hivyo Kilimba alisisitiza huku akijinasibu kwamba chama hicho hakina
wasiwasi juu ya kushinda katika uchaguzi huo mdogo kutokana na serikali
ya chama hicho kujishusha kwa wananchi wa ngazi za chini.Naye
mgombea wa chama hicho Justine Monko kwa upande wake amewahakikishia
wakazi wa jimbo hilo kwamba hataweza kuwaangusha endapo watampa ridhaa
ya kuwa mbunge wao kwa kumchagua kwa kura za kutosha na za kishindo na
hatasita kuwatumikia kwa weledi wa hali ya juu.
“Namshukuru
sana Rais wetu Dk.John Pombe Magufuli kwa kuniteua kuwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Liwale,kanipa nafasi hiyo nimejifunza mengi
sana pamoja na namna bora ya kuwatumikia wananchi”alisisitiza Monko.
No comments:
Post a Comment