Kamanda
wa Polisi Mkoani Tanga,Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Edward Bukombe
akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na matukio yaliyotokea kwa
kipindi cha mwaka mzima ambapo alisema Jumla ya Silaha 14 za moto
zilikamatwa kulia ni RCO wa mkoa wa Tanga,Justine Masejo
JESHI
la polisi mkoani Tanga, limewahadharisha wananchi kuelekea katika msimu
wa sikukuu za Krismasi na Mwaka mpya, kujiepusha na vitendo vya uvunjifu
wa amani kama ulipuaji baruti na fataki ikiwemo kuchoma moto matairi
barabarani, kwa yeyote atakayefanya hivyo atachukulia hatua za kisheri.
Kamanda
mpya wa mkoa huo, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Edward
Bukombe, alisema kwamba jeshi hilo linapiga marufuku kwa mtu yeyote
kulipua au kusababisha milipuko ikiwemo baruti, fataki na Eksozi za
magari, watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria namba 13 ya sheria ya
milipuko.
“Hivyo
wakazi wa mkoa wa Tanga, ni marufuku kuchoma matairi hovyo na kulipua
baruti bila kibali, kufanya hivyo ni kinyume cha sheria, kanuni na
taratibu za nchi. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakae
kiuka agizo hili,” alisema RPC Bukombe.
Alisema
uzoefu unaonesha kuwa siku za sikukuu watu wengi hujisahau kujiwekea
ulinzi ikiwemo kuwaangalia watoto hivyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha
wazazi kuhakikisha wanachukua hatua za kuwalinda watoto pamoja na
nyumba zao ili wahalifu wasitumie mwanya huyo kufanya uhalifu wa kuvunja
au watoto kupotea mitaani.
Kamanda
Bukombe alisema kwamba jeshi hilo limejipanga kuhakikisha kuwa wananchi
wanasherehekea sikukuu hizo kwa amani na utulivu bali aliwakumbusha
kuzingatia taratibu za kumbi za burudani kufungwa nyakati za saa 6:00
usiku na hata ibada za mkesha wa Krismasi na Mwaka mpya zimalizike muda
huo.
Katika
hatua nyingine Kamanda huyo wa polisi alisema mwenendo wa uhalifu
mkoani humo, katika kipindi cha Januari hadi Novemba mwaka 2017,
umeendelea kuwa katika hali ya amani na utulivu ma hakuna matukio
yanayotishia usalama kwa wananchi baada ya kuyadhibiti kwa kushirikiana
na vyombo vingine vya dola.
Hata
hivyo, alisema kwamba katika kipindi cha Januari hadi Novemba mwaka huu,
katika misako waliyoiendesha na operesheni mbalimbali waliweza kukamata
wahalifu waliofanya matukio mbalimbali ambapo kesi za bangi zilikuwa
237 kwa bangi yenye uzito wa kilogramu 76.1 na mirungi kesi zilikuwa 37
na uzito wa mirungi ilikuwa kilogramu 5,396.740.
Kwa
upande wa wahamiaji haramu jeshi hilo walikamata wahamiaji haramu
wapatao 224 kati ya hao Wasomali walikuwa 55 na Waethiopia walikuwa 149
na Wakenya walikuwa 20 ambao wote walifikishwa katika vyombo vya
sheria.
Kamanda
huyo pia alisema kuwa katika kudhibiti ujambazi na unyang’anyi wa
kutumia silaha, jeshi hilo katika kipindi hicho lilifanikiwa kukamata
jumla ya silaha 14 za moto ambapo bastola zilikuwa 2, shortgun 3 na
magobore yaliyotengenezwa kienyeji yalikuwa 9.
Kamanda
wa Polisi Mkoani Tanga,Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Edward Bukombe
akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na matukio yaliyotokea kwa
kipindi cha mwaka mzima ambapo alisema Jumla ya Silaha 14 za moto
zilikamatwa, kushoto ni Afisa Mnadhimu wa Jeshi hilo Mkoani Tanga,Leonce
na kulia ni RCO wa mkoa wa Tanga,Justine Masejo(Habari kwa Hisani ya
Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
Sehemu ya waandishi wa habari wakichukua taarifa
No comments:
Post a Comment