Mradi
wa majaribio wa miezi 15 wa watoto waliokosa shule, kujifunza wenyewe
kwa kutumia teknolojia ya kisasa inayotumia tableti umezinduliwa mkoani
Tanga.
Mradi huo uliozinduliwa katika kijiji cha Zenith ya Kati, wilayani
Muheza ni sehemu ya mradi mkubwa wa miaka mitano wa majaribio duniani
chini ya Global Learning Xprize wenye lengo la kutatua matatizo ya
kujifunza.
Mradi huo hapa nchini unaendeshwa kwa pamoja na Shirika la Mpango wa
Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP), Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na XPrize ambao wametoa tableti husika.
Aidha kuwezekana kuwapo kwa mradi huo kumetokana pia na makubaliano kati
ya serikali ya Tanzania kupitia Wizara yake ya elimu na TAMISEMI na
mashirika.
Katika utoaji elimu huo watoto wanaohusika ni wa miaka kuanzia 9 hadi 11
na watajifunza kwa kutumia program tano zilizowekwa katika tableti
zitakazomuwezesha kujua kusoma, kuandika na kuhesabu.
Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu akivishwa skafu na
kukaribishwa katika hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa
kutumia teknolojia kujifunza, kuandika kusoma na kuhesabu uliozinduliwa
Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning
Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP. Kushoto ni Mwakilishi wa Unesco ambaye
pia anasimamia mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo.
Mradi huo wa Tanga ambao utagusa watoto 2,400 kutoka katika vijiji 167
vya wilaya za Handeni, Korogwe, Lushoto, Muheza, Mkinga na Pangani
unatoa changamoto kwa timu ya wabunifu kuwezesha watoto walio na fursa
ndogo ya kuingia katika elimu darasani kujifunza stadi za msingi za
kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) kwa kutumia tableti wakijifunza
wenyewe.
Akizungumza katika uzinduzi wa mradi huo katika kijiji cha Zenith,
Muheza Mkoani Tanga, Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi
huo Faith Shayo alisema kwamba mradi huo unaendana na majukumu ya Unesco
ya kuhamasisha elimu jumuishi katika kuhakikisha kwamba watoto wote wa
Tanzania wakiwemo wa jamii za pembezoni zilizo nyonge zinapata fursa.
Alisema UNESCO inatekeleza majukumu yake kwa kuisaidia serikali ya
Tanzania kuwezesha kutoa elimu bora kwa wananchi wake wote na hata wale
ambao hawana uwezo wa kupata elimu kutokana na mazingira yao au maeneo
yao.
Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning
Xprize, Faith Shayo akivishwa skafu na kukaribishwa katika hafla ya
kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza,
kuandika kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa
majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na
WFP. Kulia ni Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu.
Alisema Unesco kwa kuangalia mahitaji imekuwa ikisaidia serikali ya
Tanzania katika vitu mbalimbali vya kiufundi ili iweze kufanikisha lengo
la kuwa na taifa la watu walioelimika hivyo kuwa na nafasi ya kushiriki
katika kazi za kujenga uchumi.
“Mradi huu unawapa watoto ambao hawakuwahi kujiunga na shule ya msingi,
fursa nyingine” alisema Faith na kuongeza kwamba juhudi kubwa
zinazofanywa na serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Umoja wa
Mataifa utaimarisha viwango vya weledi nchini.
Faith anasema kwamba kwa sasa japo upo kwenye majaribio utakapofanikiwa utaweza kufanyiwa kazi maeneo mengine ya Tanzania.
Aidha Mwakilishi wa WFP mkoa wa Tanga ambaye ndiye anayesimamia
utekelezaji wa programu hiyo, Xavery Njovu alisema kwamba watoto hao
wataangaliwa kwa namna ambavyo wanaelewa kila wiki, wanapoenda kuchaji
tableti zao.
Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu na Mwakilishi wa Unesco
ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo
wakiwasili katika hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa
kutumia teknolojia kujifunza, kuandika kusoma na kuhesabu uliozinduliwa
Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning
Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP.
“wakati wa kuchaji pia tunaangalia matumizi ya tableti na ufaulu wa
mtoto katika kumaliza porogramu utaonekana na kama ikionekana hasongi
mbele itaangaliwa kasoro” alisema Njovu.
Alisema kuna vijana 10 wanaojua Tehama na wamefundishwa kusaidia
wanafunzi hao katika kuhakikisha kwamba tableti hazikwami au kuharibika.
Watu hao wanaoishi vijijini hukohuko pamoja na kulipwa mishahara
wamepewa pikipiki mpya aina ya Yamaha kwa lengo la kuhakikisha wanafika
kila kata yenye wahusika na kuzungumza nao.
Pamoja na tableti hizo pia kumefungwa sola za kuchajia na seva ya kuangalia mwenendo wa watumiaji wa tableti.
Kabla ya kuzinduliwa kwa mradi huo watu 282 walifunza namna ya kuhudumia vijana hao ambao wanashiriki katika program.
Mwenyekiti wa kijiji cha Zeneth wilayani Muheza, mkoani Tanga, Juma
Killo akitoa salamu kwa XPrize, UNESCO, WFP na wageni waalikwa katika
hafla hiyo. Wa pili kulia ni Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia
mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo, Afisa Miradi wa UNESCO,
Nadia Marques (wa tatu kushoto), Ofisa Elimu wa wilaya ya Pangani,
Mbwana Mohamed (wa tatu kulia), Kaimu Ofisa Elimu Lushoto, Beatus
Kipfumo (wa pili kulia) na Mwakilishi wa WFP mkoa wa Tanga, Xavery Njovu
(kulia).
Katika mafunzo hayo wasimamizi hao ambao wanajulikana kama mama au baba
vitongoji walifunza malengo ya mradi na namna ya kuangalia mwenendo wa
watoto na mradi wenyewe.
Mgeni rasmi katika ukabidhiaji wa tableti, Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga,
Mayasa Hashimu aliwataka wazazi kuhakikisha kwamba tableti hizo
zinatumiwa na watoto kwa makusudi yaliyopangwa ili kuwa na taifa la
watoto wenye weledi mkubwa.
Alisema tableti hizo maalumu ni msaada mkubwa kwa wananchi na serikali
hivyo hawana budi kuzitunza na kuzitumia kwa makusudio husika.
“teknolojia hii inayowezesha watoto kujifunza kusoma, kuandika na
kuhesabu pasipo msaada wa mwalimu ni ubunifu wa kiwango cha juu kabisa”
alisema Mayasa na kuongeza kwamba hali hiyo itabadili kabisa fikra za
utoaji elimu na kuwakomboa watoto walio nje ya mfumo rasmi wa elimu.
Mgeni rasmi Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu (kushoto)
akitoa hotuba wakati wa hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa
kutumia teknolojia kujifunza, kuandika kusoma na kuhesabu uliozinduliwa
Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning
Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa kijiji
cha Zeneth wilayani Muheza mkoani Tanga, Juma Killo, Mchumi katika
ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza, Nelson Mwanuna pamoja na
Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning
Xprize, Faith Shayo.
Aliwataka wazazi kuunga mkono jitihada za serikali kupitia kauli mbiu ya
‘Hapa Kazi Tu’ kwa kusaidia kujenga taifa lenye uelewa mkubwa kupitia
chanzo cha sasa cha maarifa pasipo msaada wa mwalimu darasani.
Alisema msaada huo ni pamoja na kutunza vifaa vyote vya mradi na kutumiwa na wahusika bila kukosa.
Aidha alishukuru Shirika la UNESCO, XPRIZE na WFP kwa kuonesha njia na
kusema kwamba mkoa utafanya kila linalowezekana kuona mradi huo wa
majaribio unafanikiwa.
Katika makadihiano hayo watoto zaidi ya 10 walipewa tableti kwa niaba ya wenzao ambao wanashiriki katika mradi.
Mmoja wa wazazi wa watoto waliokabidhiwa tableti aliyejitambulisha kwa
jina la Musa Ramadhani alisema amefurahishwa sana na mpango huo na
kuahidi kuhakikisha kwamba anatunza kifaa hicho ili mtoto wake afaidike
nacho.
Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning
Xprize, Faith Shayo akitoa salamu za UNESCO katika hafla ya kukabidhi
tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza kuandika,
kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio
unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP.
“Mtoto wangu mimi anaitwa Amir Musa na ana miaka 9; hapa tulipo ni ndani
sana kupatiwa kifaa hicho kitatusaidia sisi maskini tuliosahaulika kuwa
katika utaratibu tena wa weledi” alisema.
Aidha alisema kwamba dhamana ya utunzaji inamuangukia yeye kwa kuwa
anaamini ni kazi yake kuhakikisha kwamba mtoto wake anapata mafanikio
kutokana na mradi huo.
Naye mama Kitongoji Hilda Hule alisema kwamba ana uhakika kwamba watoto
hao watapata maarifa na kujua kusoma kwa kasi zaidi kwa kuwa hatua za
mwanzo zilionesha hamu yao ya kutaka kujua.
Anasema kwa upande wake yeye anawaangalia watu wa kitongoji cha Zeneth
na anaamini kwamba kwa mradi huo watoto wengi watafunguka.
Mmoja wa mateknisheni wa mradi huo ambao watasaidia uwapo wa tableti na
program zake Francis Kibaja mwenye makazi yake Korogwe alisema kwamba
mfumo huo wa kitabu cha kielektroniki kinamfanya mwanafunzi ajifunze na
kujisahihisha na kama watamaliza programu mapema kutokana labda kwa
urahisi watawapangia programu ngumu zaidi ili kuwakomaza.
Mwakilishi wa WFP mkoa wa Tanga, ambaye ndiye anayesimamia
utekelezaji wa programu hiyo, Xavery Njovu akitoa salamu za WFP katika
hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia
kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi
huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia
UNESCO na WFP.
Aidha alisema kwamba tableti hizo zinagemu kwa ajili ya mtoto akichoka
na pia wakati wa mazoezi program itamwambie mtoto kama amekosea au
amepatia.
Programu zilizowekwa kwa sasa katika tableti hizo ambazo hazina uwezo wa
simu ni sawa na mtu kuanza darasa la awali na kuingia shule ya msingi.
Katika mradi huo WFP wamepewa dhamana ya kusimamia uendeshaji wa kitengo
cha lojistiki na teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama-ICT) cha
majaribio katika mazingira halisi.
Mama Kitongoji wa kijiji cha Zeneth wilayani Muheza, Hilda Hule
ambaye anajukumu la kuchaji na kutunza tableti hizo akitoa maelezo ya
namna zinavyotumika kabla ya kukabidhiwa rasmi kwa watoto wa kijiji
hicho.
Aidha jukumu lake ni pamoja na kuingiza programu katika tableti, kuanzia
vituo vya kuwekea umeme unaotokana na jua kwenye tableti hizo vijijini,
kusimamia matengenezo, marekebisho na kutoa tableti mpya kipindi chote
cha majaribio.
Uzinduzi huo ulipambwa na mambo mbalimbali ukiwemo muziki wa asili
ambapo kikundi cha JAHAZI ASILI zilitumbuiza kwa ngoma za asili za
wakazi wa Tanga na pia muziki wa singeli.
Ofisa wa Xprize naye alitumbukia katika burudani za singeli na kuwa
burudani kubwa kwa watu ambao walienda naye sambamba na kama yeye
alivyokuwa akienda sambamba na wenyeji katika zungusha.
- Mwakilishi
wa WFP mkoa wa Tanga ambaye ndiye anayesimamia utekelezaji wa programu
hiyo, Xavery Njovu akionyesha waandishi wa habari (hawapo pichani)
jinsi programu mbalimbali za kujifunzia zinavyofanya kazi kwenye tableti
hizo.Ofisa
Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu akisisitiza umuhimu wa wazazi
(hawapo pichani) kushiriki katika utunzaji wa tableti hizo kabla ya
kuzigawa rasmi. Kushoto ni Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia
mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo.
Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu (wa pili kulia)
akisalimiana na mtoto Saidi Hausi wa kijiji cha Zeneth wakati wa zoezi
la kukabidhi tableti hizo. Kulia ni Mama Kitongoji Hilda Hule mwenye
jukumu la kutunza na kuchaji tableti hizo kwa umeme wa sola na Wa kwanza
kushoto ni Mwakilishi wa WFP mkoa wa Tanga, ambaye ndiye anayesimamia
utekelezaji wa programu hiyo, Xavery Njovu na Mwakilishi wa Unesco
ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo.
Mama Kitongoji wa kijiji cha Zeneth wilayani Muheza, Hilda Hule
(kulia) akikabidhi tableti kwa mtoto Saidi Hausi huku Ofisa Elimu wa
mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu (wa pili kulia), Mwakilishi wa Unesco
ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo (wa
pili kushoto) na Mwakilishi wa WFP mkoa wa Tanga, ambaye ndiye
anayesimamia utekelezaji wa programu hiyo, Xavery Njovu (kushoto)
wakishuhudia tukio hilo wakati wa hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili
ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu
uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global
Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP.
Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu (wa pili kulia)
akisalimiana na mtoto Juma Saidi wa kijiji cha Zeneth wakati wa zoezi la
kukabidhi tableti hizo. Wanaoshuhudia tukio hilo ni kulia ni Mama
Kitongoji Hilda Hule mwenye jukumu la kutunza na kuchaji tableti hizo
kwa kutumia umeme wa sola, Mwakilishi wa WFP mkoa wa Tanga, ambaye ndiye
anayesimamia utekelezaji wa programu hiyo, Xavery Njovu (wa kwanza
kushoto), Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi wa Global
Learning Xprize, Faith Shayo (wa pili kushoto).
Tala Loubieh wa WFP akitoa maelekezo ya jinsi ya kutumia programu ya
kujifunza, kuandika kusoma na kuhesabu kwa mtoto Gabu Lakiki mara baada
ya kukabidhiwa rasmi tableti hizo kwenye hafla hiyo.
Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt
Keller akiwapongeza baadhi ya watoto wa kijiji cha Zenith ya Kati,
wilayani Muheza, mkoani Tanga waliokabidhiwa tableti hizo.
Baadhi ya wafanyakazi wa WFP wanaotoa msaada wa Tehama kwenye tableti
hizo kwa watoto wa kijiji cha Zeneth pamoja wanakijiji wakifurahi jambo
katika katika hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia
teknolojia kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza
jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa
kupitia UNESCO na WFP.
Baadhi wazazi/walezi wa watoto wa kijiji cha Zeneth wilayani Muheza
wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye hafla ya kukabidhi tableti kwa
ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza kuandika, kusoma na
kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa
na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP.
Kikundi cha ngoma cha Jahazi Asilia cha wilayani Muheza wakitoa
burudani katika hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia
teknolojia kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza
jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa
kupitia UNESCO na WFP.
Makomandoo wa Skauti wakionyesha umahiri wao wakati wa kusherehesha
hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia
kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi
huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia
UNESCO na WFP.
Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt
Keller akijumuika na watoto wa kijiji cha Zeneth kucheza SINGELI wakati
wa hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia
kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi
huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia
UNESCO na WFP.
Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt
Keller aliponogewa na SINGELI katika hafla ya kukabidhi tableti kwa
ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza kuandika, kusoma na
kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa
na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP.
Mgeni rasmi na meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto
waliowakilisha wenzao kwenye hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya
mradi wa kutumia teknolojia kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu
uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global
Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP.
- Mkurugenzi
Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE ambao ndio wafadhili
wakuu, Matt Keller akiwa kwenye picha ya pamoja na Wataalamu wa Tehama
walioajiriwa na mradi kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tableti na mifumo
yote ya kusomea zinafanya kazi inavyopaswa katika mkoa wa Tanga na
vitongoji vyake.
Wafanyakazi
wa WFP wakiwa kwenye picha ya pamoja na wataalamu wa Tehama
walioajiriwa na mradi kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tableti na mifumo
yote ya kusomea zinafanya kazi inavyopaswa katika mkoa wa Tanga na
vitongoji vyake.
No comments:
Post a Comment