Mkuu
wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akiwa akishuhudia wakina mama
wakipiga na mabanho yenye ujumbe tofauti katika uzinduzi wa jukwaa la
wanawake Wilaya ya Temeke.
Wanawake
hao ambao wamejitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo, huku sherehe hizo
zikipambwa na shamrashamra za maandamano ya vikundi mbalimbali vya
wanawake wajasiriamali.
Pia wanawake wajasiriamali walionesha kazi za mikono na ubunifu ufanywao na vikundi vyao.
Katika
uzinduzi huo ulifanyika uchaguzi wa mwenyekiti wa jukwaa la wanawake
Kiwilaya ambapo Johari Maulid Mkonde alichaguliwa rasmi kuwa mwenyekiti
wa jukwaa la wanawake wilayani Temeke.
Hata
hivyo wanawake wa Temeke wamepewa fursa kushiriki uchumi wa viwanda ili
waweze kufika malengo ya maendeleo endelevu ya 50/50 ya dunia kufikia
mwaka 2030.
Jukwa
la wanawake liliundwa ili kuwawezesha wanawake kiuchumi na kuondoa
pengo kubwa ambalo limejengeka duniani na kuongeza ushiriki wa wanawake
katika uchumi duniani kote. Majukwaa haya yatazinduliwa katika Mikoa
yote nchini na Halmashauri zote. Katika Mkoa wa Dare Es Salaam Wilaya ya
Temeke ni Wilaya ya kwanza kuzindua jukwaa la wanawake.
Kauli mbiu katika uzinduzi huu ni ''Mwanamke Tumia Fursa Kushiriki Uchumi wa Viwanda''
No comments:
Post a Comment