November 22, 2017
Taasisi ya APHTA yatekeleza Vyema Mpango wa Kuzuia Magonjwa Yasiyoambukiza Mashuleni
Inaelezwa kwamba hadi kufikia mwaka 2020 magonjwa yasiyoambukiza yanaweza kusababisha asilimia 73 ya vifo kote duniani ikiwa hatua madhubuti hazitachukuliwa katika kupambana na magonjwa hayo ikiwemo Kisukari.
Ni kutokana na athari za magonjwa hayo, Chama cha Watoa Huduma za Afya Tanzania APHTA, kikazimia kuanzisha Mpango wa Kitaifa wa Afya Mashuleni, lengo likiwa ni kupambana na magonjwa hayo ambapo mpango huo unafadhiriwa na Taasisi ya “World Diabetes Foundation” ya nchini Canada.
Na sasa mpango huo unatekelezwa vyema, fuatilia video hii. Meneja Miradi kutoka taasisi ya Word Diabetes, Bent Lautrup-Nielsen (kushoto), akizungumza kwenye ziara ya kujionea utekelezaji wa mpango huo mkoani Shinyanga. Wanafunzi wa shule ya Msingi Town Mjini Shinyanga, wakiimba Ngonjela wakati wa ziara hiyo. Viongozi mbalimbali kwenye ziara hiyo. Wanafunzi wa shule ya Msingi Bugoyi B, Mjini Shinyanga wakiimba wakati wa ziara hiyo. Meneja Miradi kutoka taasisi ya Word Diabetes, Bent Lautrup-Nielsen, akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Bugoyi B, Mjini Shinyanga Meneja Miradi kutoka taasisi ya Word Diabetes, Bent Lautrup-Nielsen (katikati), akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Bugoyi B Mratibu wa APHTA Kanda ya Ziwa, Dr.Joyce Mwihava akizungumza baada ya kuwasili shule ya msingi Isenga D, iliyopo Ilemela Jijini Mwanza, wakati wa ukaguzi wa mradi wa kuzuia magonjwa yasiyoambukiza mashuleni. Meneja Miradi kutoka taasisi ya Word Diabetes, Bent Lautrup-Nielsen, akizungumza na wanafunzi wa shule ya Msingi Isenga D Jijini Mwanza. BMG Habari, Pamoja Daima
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment