Pages

November 16, 2017

RAIS MSTAAFU DKT. JAKAYA KIKWETE AONGOZA MAHAFALI YA 10 YA CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ELIMU (DUCE) CHA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM



NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MKUU wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete, (pichani juu), ameongoza mahafali ya kumi (10), ya  Chuo kikuu kishiriki cha Elimu (DUCE) cha Chuo kikuu Dar es salaam kwenye viwanja vya chuo hicho, Chang’ombe jijini Dar es Salaam  Novemba 15, 2017.
Katika mahafali hayo zaidi ya wanachuo 1,443 waliochukua mafunzo ya Shahada ya Elimu ya Jamii na Elimu, (BAED), Shahada ya Elimu ya Sayansi na Elimu, (Bsc) na Shahada ya Elimu (BED), pamoja na wahitimu waliojiendeleza (Post graduate), 
walitunukiwa shahada ya kwanza, ambapo mwanachuo Dadi Omary Safari, alipewa tuzo ya kuwa mwanachuo bora zaidi kitaaluma.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete akimpongeza mmoja wa wahitimu wa Shahada ya Elimu ya Jamii na Elimu (BAED) Amisa Hassan.
Baadhi ya wahitimu katika mahafali ya 10 ya ya  Chuo kikuu kishiriki cha Elimu (DUCE) cha Chuo kikuu Dar es salaam wakiwa kwenye mahafali hayo
Furaha ya kuhitimu na kutunukiwa shahada.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala akisoma hotuba yake.
Dkt. Kikwete akipitia ratiba ya mahafali hayo.
Dkt. Kikwete akitangaza kuwatunuku shahada baadhi ya wanachuo hao.
Baadhi ya wanachuo wakisubiri kutunukiwa shahada zao na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete.
Dkt. Kikwete akiteta jambo na Profesa Mukandala.
Dkt. Kikwete, akiipitia tuzo ya mwanachuo bora kitaaluma Dadi Emmanuel Safari kabla ya kumkabidhi.
Mwanachuo bora kitaaluma Dadi Emmanuel Safari akiwa na tuzo yake.
 
Dkt. Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mmoja wa wahitimu, Amisa Hassan na baba mdogo wa muhitimu huyo, Khalfan Said.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...