Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza wakati wa Mkutano wa
hadhara uliofanyika katika kijiji na kata ya Chiungutwa, Wilaya ya
Masasi Mkoani Mtwara mara baada ya kushiriki mnada wa tano wa Korosho. Picha na Mathias Canal
Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Gasper Byakanwa akimuonyesha Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa jinsi magunia yalivyopangwa kwa
ustadi ktika gala la kuhifadhia Korosho la Mtanda mara baada ya Mkutano
wa hadhara uliofanyika katika kijiji na kata ya Chiungutwa, Wilaya ya
Masasi Mkoani Mtwara mara baada ya kushiriki mnada wa tano wa Korosho.
Badhi
ya wakulima wa zao la korosho wa Chama cha Ushirika cha Masasi-Mtwara
Cooperative Union Ltd (MAMCU) wakifatilia mnada wa tano wa korosho
katika kijiji na kata ya Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara.
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe
Gelasius Gasper Byakanwa wakiwasili Kijijini Chiungutwa, Wilaya ya
Masasi Mkoani Mtwara kwa ajili ya kujionea Mnada wa Korosho
unavyoendeshwa.
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe. Mary Mwanjelwa (wa tatu kutoka kulia) akiwa katika
picha ya pamoja na wazee maarufu wa kijiji cha Chiungutwa, Wilaya ya
Masasi Mkoani Mtwara, wengine ni Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa (Wa kwanza kushoto), na Mbunge wa Jimbo la Mtwara
Vijijini Mhe. Hawa Ghasia (Wa kwanza kulia).
Naibu
Waziri wa Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akiteta jambo na Mkuu wa mkoa wa
Mtwara, Gelasius Byakanwa wakati wa mnada wa tano wa Korosho.
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akiwa na Mbunge wa Jimbo la Mtwara
Vijijini Mhe Hawa Ghasia wakati wa ukaguzi wa ghala la Buko kijijini
Chiungutwa wilaya ya Masasi mkoani Mtwara wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisikiliza ushauri sambamba na
pongezi kwa kushiriki mnada wa tano wa Korosho kijijini Chiungutwa, wilaya ya Masasi mkoani Mtwara wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo.
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe
Gelasius Gasper Byakanwa wakikagua magunia ambayo tayari yamewasili
katika Ofisi ndogo ya makao Makuu ya Chama Kikuu cha ushirika
mara baada ya kumalizika kwa mnada wa tano wa Korosho Kijijini
Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara.
Na Mathias Canal, Mtwara
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Mary Machuche Mwanjelwa leo Novemba 18, 2017
amemuagiza Mrajisi wa vyama vya ushirika kukamilisha haraka kazi ya
uchunguzi kwenye Bodi za vyama vya ushirika vya Mkoa wa Mtwara ili
kubaini sababu zilizopelekea kuuzwa kwa magunia kiholela.
Alisema
kuwa kumalizika kwa uchunguzi huo kutarahisisha kuchukuliwa haraka
hatua kali za kisheri kwa wale wote watakaobainika kukiuka sheria No 17
ya vyama vya ushirika.
Naibu
waziri alitoa agizo hilo wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika
katika kijiji na kata ya Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara mara
baada ya kugundua kuwa kuna viashiria vya ukiukwaji wa taratibu katika
upatikanaji wa magunia ya kuhifadhia korosho wakati wa ziara yake ya
kikazi Mkoani humo.
Sambamba
na hilo Naibu waziri Mhe Mwanjelwa wakati wote wa mkutano huo
ameshuhudia malalamiko kutoka kwa wakulima wa zao la korosho wa Chama
cha Ushirika cha Masasi-Mtwara Cooperative Union Ltd (MAMCU) kuhusu
ucheleweshwaji wa upatikanaji wa maguni kutoka kwa mzabui, Mapungufu ya
kilo kati ya PDA na WHRs ghala kuu, ikiwa ni pamoja na kuchelewa kwa
malipo ya wakulima kwa njia ya benki kutoka kwa wanunuzi.
Katika
ziara yake hiyo kilio cha wananchi wengi na wakulima walisiitiza zaidi
kuhusu kukosekana kwa magunia hayo huku wakieleza kuwa wakati mwingine
kuchelea kufika ama kutowafikia kabisa jambo ambalo linachangia
kupunguza thamani ya zao la korosho.
“Nataka
Mrajisi ufanye na ukamilishe kazi yako ya uchunguzi na baada ya kuipata
taarifa hiyo hatua stahiki zitachukuliwa kwa wale wote watakaogundulika
kukiuka sheria ya nchi” Amekaririwa Naibu Waziri Mhe Mwanjelwa
Mbali
na agizo hilo Naibu Waziri pamoja na wabunge wa Mkoa wa Mtwara walipata
nafasi ya kujionea mnada wa tano wa ununuzi wa korosho unavyoendelea.
Hata hivyo Mnada wa tano ulishuhudiwa Kilogramu 7,524,104 za korosho zikiuzwa kwa thamani ya zaidi ya Bilioni 30.
Wakati
huo huo Naibu Waziri Mhe Mwanjelwa amesema Wizara itayafanyia kazi
haraka mapendekezo ya tume iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe
Gelasius Byakanwa kufanya uchunguzi kuhusu mwenendo mzima wa
magunia pamoja na upatikanaji wake.
No comments:
Post a Comment