Aliyekuwa Mhasibu wa Taasisi ya Kuzuiana Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Godfrey Gugai amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo na kusomewa jumla ya mashtaka 44 likiwamo la kumiliki mali nyingi zisizolingana na kipato chake.
Mhasibu huyo anadaiwa kumiliki viwanja 37, maghorofa 7, nyumba za kawaida 9, magari 5 pamoja na pikipiki, pamoja na kutakatisha fedha, kughushi fedha na kudanganya kuhusu mali ambazo anamiliki.
Jana Gugai alijisalimisha Makao Makuu ya TAKUKURU baada ya Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bregedia Jenerali John Mbun'go kutangaza dau la milioni 10 kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwake.
No comments:
Post a Comment