Meza
kuu kutoka kushoto ni Balozi Liberata Mulamula, Balozi wa Tanzania
nchini Marekani na Canada Mhe. Wilson Masilingi, Naibu Waziri wa afya
Zanzibar, Mhe. Harusi Said Suleiman,Mkuu wa kitengo cha Diaspora Wizara
ya mambo ya nje na ushirikiano Afrika Mashariki, Balozi Anisa Mbega,
Bi.Adila Hilal Vuai mkurugenzi wa Idara ya ushirikiano wa kimataifa na
uratibu wa wazanzibari wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) !,
Bwn. Assenga kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Dr. Ali
Salum Ali Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar.
wakifuatilia jukwaa la afya lililoandaliwa na DICOTA katika
kuwakutanisha wadau wote nje na ndani ya Marekani sekta ya afya
kuwatambua na kuthamini mchango mkubwa wanaotoa katika sekta hiyo nchini
Tanzania. Jukwaa la afya lilifanyika siku ya Jumamosi Novemba 11, 2017
Martins Crosswind Greenbelt, Maryland nchini Marekani. Picha naVijimambo
Blog na Kwanza Production
Bwn. Lunda Asmani akiwakaribisha wadau wote na kufungua jukwaa la afya.
Balozi
wa Tanzania nchini Marekani na Mexico akisoma hotuba yake kwenye
kongamano la Afya lililofanyika siku ya Jumamosi Nov 11, 2017 Greenbelt,
Maryaland nchini Marekani. Katika hotuba hiyo aliwashukuru DICOTA kwa
kuandaa jukwaa hilo la wadau wa afya kwa kuthamini kazi kubwa
inayofanywa na wadau hao na jitihada binafsi zinazofanywa kwa kusaidia
ndungu zao nyumbani Tanzania pia alisema Rais Dkt John Pombe Magufuli
anatambua na kuthamini mchango mkubwa unaofanywa na Diaspora kwa nchi
yao.
Balozi
wa African Union nchini Marekani, Mhe.Arikana Chihombori Quao
akichangia kwenye jukwaa hilo na kueleza changamoto nyingi nchi za
Afrika inazopata katika sekta hiyo kutokana na miundo mbinu kuwa duni na
sababu kubwa inachangiwa na wakoloni walivyoligawa bara la Afrika na
kuwa nchi mbalimbali kwa kuogopa nguvu ya Afrika na utajiri wake usije
ukaongoza Dunia.
Naibu
Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe. Harusi Said Suleiman akiwashukuru
Diaspora kwa mchango mkubwa kwa sekta ya afya Zanzibar na baadae kutoa
salamu za Rais wa Zanzibar Mhe. Dr Ali Mohamed Shein kwa kutoa shukurani
zake na kuthamini mchango mkubwa wa Diaspora hasa katika sekta ya Afya.
Balozi
Anisa Mbega mkuu wa idara ya Diaspora Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki akishiriki jukwaa la Afya kwa
kuwapongeza DICOTA kwa kuandaa jukwaa hilo na kuwakutanisha wadau wa
afya na Serikali inathamini na kutambua mchango mkubwa unaofanywa na
Diaspora.
Balozi
Liberata Mulamula akitoa shukurani zake kwa DICOTA kwa kuandaa jukwaa
la afya na baadae kutoa mfano wa mtu akiwekewa fedha na afya bora yeye
atakimbilia kwenye fedha kwa sababu hatambui umuhimu wa afya njema ni
zaidi ya fedha kwa maana kwamba binadamu wengi hawaelewi umuhimu wa afya
lazima tutambue hilo huku akitolea mfano mwingine wa nyani unapo mwekea
fedha na ndizi yeye atachangau ndizi kwa sababu anajua bila ndizi
maisha yake yapo hatarini.
Dr.
Mary Banda kutoka Jambo Tanzania akielezea jinsi alivyotumia elimu yake
kwa kuelekeza nguvu yake kusaidia sekta ya afya mkoa wa Kagera.
Bi.
Christine Lasway kutoka MyAfyaPal akielezea umuhimu wa afya na jinsi
anavyoelekeza nguvu zake katika kusaidia sekta ya afya nchini Tanzania.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Bi.Tausi
Suedi kutoka Childbirth Survival Tanzania akielezea jinsi alivyojikita
katika kusaidia kuokoa maisha ya mtoto hasa wakati wa uzazi Tanzania kwa
kutoa elimu kwa wakunga na wazazi kabla na baada ya kujifungua ikiwemo
kwapelekea mahitaji muhimu kabla ya kujifungua.
Dr.
Secelela Malecela kutoka Janet Weir Children's Hospital akieleza
anavyoguswa katika kuelekeza nguvu zake katika sekta hiyo Dodoma.
Bi. Adila Hilal Vuai mkurugenzi wa Idara ya ushirikiano wa kimataifa na uratibu wa wazanzibari wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) akitoa
shukurani kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa jitihada za
Diaspora katika sekta ya afya Zanzibar na kuwapongeza DICOTA kwa kuandaa
jukwaa la Afya na kuwaasa kutumia lugha ya Kiswahili katika kuendeleza
na kuthamini utamaduni wetu.
Dr.
Frank Mimja akielezea umuhimu wa kusaidia sekta ya afya Tanzania na
jitihada anazofanya kwa kupeleka madaktari Tanzania na kuwaelekeza wadau
waliohudhuria jukwaa la Afya njia iliyosahihi kupitia katika kutimiza
ndoto na azma yako ya kusaidia ndugu zetu Tanzania.
Kutoka
kushoto ni Bwn. Lunda Asmani DICOTA, Bi. Adila Hilal Vuai kutoka Ofisi
ya Rais Zanzibar na Dr. Ali Salum Ali Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya
Mnazi Mmoja Zanzibar.
Juu na chini ni wadau wa jukwaa la afya wakifuatilia jukwaa hilo wakati likiendelea.

Post a Comment