Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Mhe. Seleman Jafo
akizindua kampeni ya kitaifa ya uanzishwaji wa viwanda
vidogo na vya kati katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za
Mitaa kwenye kikao cha Maafisa wa maendeleo ya jamii wa mikoa na Halmashauri
kilichofanyika katika ukumbi wa chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Mjini
Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Mhe. Seleman Jafo
akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Binilith Mahenge muongozo wa
uanzishwaji wa viwanda vidogo na kati wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya
uanzishwaji wa viwanda vidogo na kati katika Mikoa na Mamlaka za Serikali
za Mitaa katika Kikao cha Maafisa maendeleo ya jamii wa Mikoa na
Halmashauri kilichofanyika katika ukumbi wa chuo cha Mipango ya Maendeleo
vijijini , mjini Dodoma
Baadhi ya Wakuu wa Mkoa kutoaka Mkoa wa Iringa, Singida, Manyara
,na Morogoro wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Mhe.
Seleman Jafo(Hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya uanzishwaji wa
viwanda vidogo na kati katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa
katika Kikao cha Maafisa maendeleo ya jamii wa Mikoa na Halmashauri
kilichofanyika katika ukumbi wa chuo cha Mipango ya Maendeleo vijijini , mjini
Dodoma
........................................................................................................................
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa Mhe. Selemani Jafo amezindua kampeni ya uanzishwaji wa viwanda vidogo na
vya kati katika Mamlaka za serikali za Mitaa na kuwataka wakuu wa mikoa kuhakikisha
wanatimiza azma ya serikali ya kuhamasisha na kuanzisha viwanda hivyo kwenye
maeneo yao.
Jafo amezindua kampeni hiyo ya kitaifa leo katika ukumbi wa
chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini
Mjini Dodoma na kuhudhuriwa na Maafisa wa maendeleo ya jamii wa mikoa na
Halmashauri, Wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi na viongozi mbalimbali.
Waziri Jafo amesema kila Mkuu wa mkoa anawajibu wa kuhakikisha
azma ya serikali ya uchumi wa viwanda inatekelezwa kwenye eneo lake na kwamba
watapimw utendaji wao wa kazi kupitia ajenda ya viwanda.
Amewataka Wakuu wa Mikoa nchini kuwahamasisha Mamlaka za
Serikali za Mitaa kuainisha na kutenga maeneo rafiki ya uwekezaji ili
wawekezaji wanapokuja waweze kuonyeshwa maeneo kwa haraka ambapo
itasaidia kukuza uchumi katika ngazi ya Serikali za Mitaa.
“Kila Mkuu wa Mkoa atapimwa kulingana na viwanda ambavyo
vimezalishwa katika mkoa wake kulingana na agenda ya kukuza uchumi wa viwanda
nchini lengo likiwa kuunga mkono juhudi za Serikali za kukuza uchumi na
kupunguza umaskini kwa wananchi” Amesema Mhe. Jafo.
Amesema katika mwaka wa fedha 2016/2017 Halmashauri
zote nchini zilitenga shilingi bilioni 53 kwa ajili ya kuwawezesha vijana na
wakina mama, zilizotolewa hadi juni, 2017 ni shilingi bilioni 15.5 na
tayari asilimia kumi zilishatolewa kwa vijana na akina mama wajasiriamali
nchini lengo likiwa ni kuwawezesha kiuchumi na kupunguza umaskini nchini.
Mhe. Jafo amesema wakuu wa Mikoa wote nchini wanatakiwa kuwaongoza
wananchi katika kuanzisha viwanda vidogo na vya kati ili kuweza kukuza uchumi
na kuongeza ajira nchini na kupunguza umaskini kuanzia ngazi ya kaya hadi taifa
kwa ujumla.
Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe.Jenista Mhagama
amesema uchumi wa nchi umeendelea kukua lakini tatizo la ajira bado lipo
nchini, kwa kuwa ajira rasmi imekuwa ikitoa asilimia 13 ya ajira zote katika
nchi yetu na asilimia nyingine zimejikita katika sekta isiyo rasmi na
sekta ya kilimo.
Amesema kuwa sekta isiyorasmi inajumuisha wananchi wenye
kipato cha kati na chini wanaojishughulisha na kilimo, uvuvi,
misitu na shughuli ndogondogo katika jamii, hivyo ili kuweza kupambana na
upungufu wa ajira nchini ni lazima kutekeleza dira ya maendeleo ya mwaka 2025
inayoenda kwenye uchumi wa viwanda kuwa nimsingi wa kuondokana na umaskini
nchini.





إرسال تعليق