Na Pamela Mollel,Monduli
Katibu
Mkuu wa wizara ya ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Dokta Florens
Turuka amesema kuwa jeshi hilo hivi sasa limejipanga katika kukabiliana
na changamoto za ulinzi na usalama kwa
kuwapatia askari wake mafunzo maalumu ya sayansi ya kijeshi.
Aliyasema
hayo Jana wakati akizungumza katika uzinduzi wa shahada ya kwanza ya
sayansi ya kijeshi inayotekelezwa na chuo cha uhasibu Arusha kwa
kushirikiana na Chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli (TMA).
Alisema
kuwa, kumekuwepo na matishio mengi ambayo yamekuwa yakijitokeza Kwa
namna tofauti ambapo hivi sasa matishio hayo yamegeuka na kuhamia kwenye
mitandao, hivyo kama jeshi wana wajibu wa kujipanga zaidi kwa kuwaandaa maaskari ili waweze kukabiliana na hali hiyo mahali popote.
Dokta
Turuka alisema kuwa, wao Kama jeshi ni wajibu wao kujipanga mapema kwa
kuangalia namna ya kuwajengea uwezo hasa katika maswala ya sayansi na
teknolojia ili kuboresha ulinzi na usalama hapa nchini.
Kwa
upande wa Mkuu wa majeshi nchini, Jenerali Venance Mabeyo alisema kuwa
wamekuwa wakitoa mafunzo hayo kwa maaskari wake kulingana na mabadiliko
ya kidunia hasa katika maswala ya
sayansi na teknolojia kwani ni eneo ambalo linahitaji elimu kubwa
zaidi. Alisema kuwa, ni lazima wasonge mbele na kwenda na wakati kwani
wasipofanya hivyo watabaki nyuma na kamwe hawataweza kukabiliana na
vitisho vilivyopo hivi sasa.
Naye
Mkuu wa chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli (TMA), Dokta Paul Massao
alisema kuwa, wamekuwa wakitoa masomo ya kijeshi na kiraia ili kuwaandaa
vijana katika hatua ya ngazi za juu zaidi kielimu ambapo kwa kuanzia kozi hiyo watahiniwa 158 wataanza kozi hiyo mapema.
Kwa
upande wa Kaimu mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha, Dokta Faraji Kasidi
alisema kuwa, mahusiano kati yao na chuo hicho cha kijeshi yameanza muda
mrefu ambapo wao wamekuwa wakifundisha askari hao mafunzo ya kiraia ambayo yamekuwa yakileta manufaa makubwa Sana.
Katibu
Mkuu Wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga Taifa Florens Turuka
akisalimia na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Iddy Kimanta mara baada ya
kuwasili katika chuo cha mafunzo ya kijeshi Mondoli(TMA) kwa ajili ya uzinduzi wa shahada ya kwanza ya mafunzo ya Sayansi ya kijeshi
iliyofanyika chuoni hapo leo(Picha na Pamela Mollel Arusha)
Mkuu
wa majeshi ya ulinzi na usalama Tanzania Jenerali Vanance Mabeyo
akisalimiana na Kaimu Mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha Dokt Faraji
Kasidi, katikati ni Mkuu wa chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli (TMA),
Dokta Paul Massao
Katibu
mkuu wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga Taifa Florens Turuka
akisalimia na Meja Jenerali Othman mara ya kuwasili katika chuo cha
mafunzo ya kijeshi Mondoli(TMA) kwa ajili ya uzinduzi wa mafunzo ya
shahada ya kwanza ya Sayansi ya kijeshi iliyofanyika chuoni hapo.
Katibu
mkuu wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa Florens Turuka
akisalimiana na Dr. Adolf B. Rutayuga ambaye ni kaimu mtendaji mkuu wa
NACTE.
Katibu
mkuu wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa Florens Turuka
akizungumza katika uzinduzi wa uzinduzi wa shahada ya kwanza ya Sayansi
ya kijeshi iliyofanyika chuoni hapo
Mkuu
wa majeshi nchini, Jenerali Venance Mabeyo akitoa hotuba fupi katika
halfa ya uzinduzi wa mafunzo ya shahada ya kwanza ya Sayansi ya kijeshi
iliyofanyika chuoni hapo
Meja jenerali Paul Peter Masao ambaye ni mkuu wa chuo cha mafunzo ya maafisa wanafunzi jeshi la ulinzi la Tanzania(TMA).
Mwenyekiti
wa Bodi ya chuo cha uhasibu Arusha Bi.Rukia Adam akisoma maelezo mafupi
juu ya uzinduzi wa wafunzo ya shahada ya kwanza ya sayansi ya kijeshi
inayotekelezwa na chuo cha uhasibu Arusha kwa kushirikiana na Chuo cha
mafunzo ya kijeshi Monduli (TMA).
Kaimu
mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha, Dokta Faraji Kasidi akizungumza katika
uzinduzi huo ambapo alisema mahusiano kati yao na chuo hicho cha kijeshi
yameanza muda mrefu ambapo wao wamekuwa wakifundisha askari hao mafunzo ya kiraia.
kushoto aliyevalia suti ni Profesa Johannes Monyoambaye aliwahi kuwa mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha(IAA)
Wanafunzi wa mafunzo ya shahada ya kwanza ya Sayansi ya kijeshi iliyofanyika chuoni hapo leo
Maafisa wa jeshi wakitumbuiza wata wa uzinduzi wa wafunzo ya sayansi ya kijeshi.
Picha ya pamoja
No comments:
Post a Comment