Muonekano wa Barabara
ya Sumbawanga-Matai-Kasanga KM 112, mkoani Rukwa, ambayo ujenzi wake
unatarajiwa kukamilika mwakani.
|
Muonekano wa barabara
ya kuruka na kutua ndege katika Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga, Mkoani Rukwa. Upanuzi
wa Uwanja huo unatarajiwa kuanza mapema mwezi Ujao.
|
Muonekano wa Barabara
ya Sumbawanga-Matai-Kasanga KM 112, mkoani Rukwa, ambayo ujenzi wake
unatarajiwa kukamilika mwakani.
|
Muonekano wa eneo
korofi katika sehemu ya Barabara ya Matai-Kasanga, mkoani Rukwa, ambayo ujenzi
wake unatarajiwa kukamilika mwakani.
|
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema ujenzi wa uwanja wa ndege
wa Sumbawanga utaanza kujengwa kwa kiwango cha lami kuanzia mwishoni mwa mwaka
huu baada ya taratibu za kumpata mkandarasi kukamilika.
Akizungumza na
wananchi wanaozunguka Uwanja huo Prof. Mbarawa amewahakikishia wananchi wote wanaostahili kulipwa fidia
kutokana na kupisha ujenzi huo watalipwa fidia zao katika kipindi kisichozidi
miezi miwili kuanzia sasa.
“Jumla ya wananchi 97,
ndio wanaostahili kulipwa fidia na kiasi cha shilingi bilioni 3.3 kimetengwa na wataanza kulipwa hivi karibuni
kabla ya zoezi la ujenzi wa uwanja huo kuanza” amesema Prof. Mbarawa.
Amewataka wananchi hao
kuacha kupita katika uwanja huo kwani ni hatari
kwa usalama wa ndege na usalama wa wananchi wenyewe.
Ujenzi wa uwanja wa ndege
wa Sumbawanga unajengwa kwa kiwango cha lami na kuongezwa urefu kutoka kilomita
1.5 had 1.7 ili kuwezesha ndege kubwa zaidi kutumia uwanja huo na hivyo
kuufungua mkoa wa Rukwa na mikoa mingine hali itakayochochea maendeleo na
ukuaji wa uchumi kwa mkoa huo.
Kaimu Meneja wa
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Mkoa wa Rukwa, Mussa Mchola amemshukuru Waziri Prof.
Mbarawa kwa hatua ya kulipa fidia na kumhakikishia kuwa watamsimamia mkandarasi
huyo kikamilifu ili ujenzi huo ukamilike kwa wakati na kwa ubora unaostahili.
Katika hatua nyingine
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Mbarawa amekagua Ujenzi wa
Barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasanga Port KM 112 na mizani ya Singiwe na
kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa miradi hiyo ambapo amemtaka mkandarasi China Railway 15, Bereau Group Corporation (CR15G) na Henan Provincial Newcentry Road na Bridge
Consultants Limited JV anaejenga kuongeza kasi katika maeneo korofi kabla ya
Mvua za masika kuanza.
Naye Mkuu wa Wilaya ya
Kalambo, Mwl. Julieth Binyura amezungumzia umuhimu wa ukamilishaji wa barabara
hiyo utakavyonufaisha wilaya hiyo kwa kuwa inaunganisha Wilaya hiyo na bandari
ya Kasanga na mpaka wa Kasesha unaounganisha Tanzania na Zambia na hivyo
kuchochea uzalishaji na uchukuzi kati ya Tanzania, Kongo na Zambia.
Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano iko katika mchakato wa kuunganisha kwa kiwango cha lami
barabara zinazoingia katika bandari za mipakani ili kukuza huduma za uchukuzi
kati ya Tanzania na nchi jirani kwa njia za magari, ndege na meli.
Imetolewa na Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
No comments:
Post a Comment