Na Stella Kalinga, Simiyu
Waziri
wa Kilimo Mhe.Dkt. Charles Tizeba amewataka wamiliki wa viwanda vya
kuchambua pamba(ginners) kupeleka pamba mbegu kwenye kiwanda cha
kuchakata(kutoa manyoya) mbegu za pamba cha Quton na akasema watakaogoma
kupeleka hawatanunua pamba msimu ujao.
Waziri
Tizeba ameyasema hayo jana alipotembelea kiwanda hicho katika Kata ya
Kasoli wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu kwa lengo la kujionea hali ya
uzalishaji wa mbegu ya pamba inavyoendelea.
Amesema
suala la wenye viwanda vya kuchambua pamba(ginners) kupeleka pamba
mbegu katika kiwanda cha kuchakata mbegu za pamba(kuondoa manyoya) siyo
la hiari na walishapewa maelekezo, hivyo wanapaswa kupeleka pamba mbegu
katika kiwanda cha Quton ili zitolewe manyoya na baadaye zipelekwe kwa
wananchi.
“
Nimeambiwa watu wa Quton wanashindwa kufanya kazi kwa shift tatu kwa
siku kwa sababu walio na mbegu kwenye viwanda vyao vya kuchambua pamba
hawataki kuleta pamba hapa, wakati wanayo maelekezo na hii siyo hiari
mbegu ikishatengwa na Bodi ya Pamba si yao” alisema Tizeba.
“Mkurugenzi
wa Bodi ya Pamba nakuagiza wapelekee ujumbe huu kwamba ginner
atakayegoma kuleta pamba mbegu hapa Quton hanunui pamba mwaka kesho,
wanapaswa walete mbegu zitolewe manyoya ziende kwa wananchi ili wapate
mbegu bora, katika hili sitabembelezana na mtu” alisisitiza Tizeba.
Aidha,
Mhe.Waziri amesema mahitaji ya mbegu ya pamba iliyotolewa manyoya kwa
nchi nzima ni takribani tani 8000, hivyo ili kufikia kiwango hicho
katika siku zilizobaki kuelekea msimu wa kilimo cha pamba, kiwanda cha
Quton kinapaswa kufanya kazi saa 24 kwa kuwa uzalishaji wa sasa wa tani
60 hadi 65 kwa saa 16 kwa siku hautaweza kufikia lengo hilo.
Wakati
huo huo Waziri Tizeba ametoa wito kwa wananchi Mkoani Simiyu kutopanda
pamba sasa kwa kuhofia mvua kukatika mapema, badala yake wasubiri
taarifa rasmi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa juu ya hali ya mvua katika
ukanda huo itakayotolewa muda mfupi ujao,ambayo baadaye itatumika
kuwashauri wakati muafaka wa kupanda, japo alieleza kuwa taarifa ya
jumla ya utabiri wa hali ya hewa inaonesha mvua itanyesha juu ya
wastani.
Pia
Mhe.Waziri amewahakikishia wananchi kuwa bei ya mbolea imeshuka, hivyo
akawataka wataalam wa Kilimo kuwaelimisha wananchi juu ya bei elekezi ya
mbolea kwa kila wilaya, ili wasiuziwe kwa bei kubwa na akasisitiza kuwa
bei ya mbolea na mbegu mwaka 2018 itapungua zaidi kwa kuwa Serikali
imefuta takribani kodi 80 katika kilimo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga amesema Mkoa wa
Simiyu unazalisha pamba kwa wingi, ambapo katika msimu wa mwaka
2016/2017 umezalisha takribani asilimia 65 ya pamba ya nchi nzima, hivyo
akaomba wananchi wa mkoa huo wasaidiwe kupewa mikopo ya zana bora za
kilimo na pembejeo nyingine kupitia mfuko wa pembejeo ili kuongeza
uzalishaji zaidi.
Naye
Mkurugenzi wa Kampuni ya Quton Tanzania Limited Ndg. Pradyumansinh
Chauhan amemuomba Waziri wa Kilimo kuhamasisha wananchi kutumia mbegu za
pamba zilizotolewa manyoya ili kuongeza uzalishaji kwa kuwa
hazishambuliwi kwa urahisi na magonjwa na zinapunguza kiasi cha mbegu
kinachotumika shambani ambapo kilogramu sita tu hutumika kwa hekali
wakati zenye manyoya hutumika hadi kilogramu 15.
Waziri
wa Kilimo, Mhe.Dkt.Charles Tizeba (wa tatu kushoto) akisikiliza maelezo
kutoka wa Meneja Uzalishaji wa Mbegu,Pheneas Chikaura(kulia) katika
Kiwanda cha Kuzalisha mbegu za pamba cha Quton wakati wa ziara yake
kiwandani hapo Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.
Waziri
wa Kilimo, Mhe.Charles Tizeba akikaribishwa na Mkurugenzi wa Quton
Tanzania Limited Ndg.Pradyumansinh Chauhan, alipotembea Kiwanda cha
kuzalisha Mbegu za Pamba cha Quton kilichopo kata ya Kasoli Wilayani
Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi
wa Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance Ginnery, Ndg. Boazi
Ogola(wa pili kushoto) akimuongoza Waziri wa Kilimo, Dkt.Charles Tizeba
(aliyeweka mkono kifuani) na baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya Bariadi na
Mkoa wa Simiyu kuelekea kuona kiwanda hicho wakati wa ziara ya Waziri
huyo Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Quton Tanzania Limited, Ndg.Pradyumansinh Chauhan akitoa
taarifa ya uzalishaji wa mbegu za pamba zilizotolewa manyoya katika
kiwanda cha kampuni hiyo kwa Waziri wa Kilimo, Mhe.Dkt.Charles Tizeba
alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi
Mkoani Simiyu.
No comments:
Post a Comment