Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii
Serikali
ya Marekani kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania leo imezindua
kituo kipya cha kimarekani kitakachokuwa kitovu cha uvumbuzi na ubunifu
wa teknolojia kakinacholenga kukuza fikra yakinifu na mijadala ya kina
kuhusu masuala mbali mbali ya kuwapa wananchi haki ya kupata elimu na
kupata taarifa bila kikwazo.
Kituo
hicho kitakuwa ni daraja la kuzifikia taasisi za elimu ya juu za
Kimarekani, taasisi za utafiti, za kimarekani, na hata ufadhili wa
masomo na kushirikisha hulka ya ubunifu na ujasiriamali kwa watanzania
watakaobuni mustakabali mpya.” Tunawekeza
Akizungumza kwenye uzinduzi wa kituo hicho, Kaimu balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dk. Inmi Patterson amesema,
kituo hicho kipya kitakuwa kiunganishi cha kidijitali kati ya Tanzania
na eneo la Silicon Valley (kitovu cha uvumbuzi na ubunifu wa
teknolojia)Tehama na ubunifu.
Dk.Patterson
amesema Vituo vya Kimarekani ni maeneo yaliyotengwa maalumu katika
taasisi mbalimbali za nchini Tanzania “kituo hiki cha lugha ya
kiingereza tunachofungua leo kitatoa uwezo wa moja kwa moja wa kujifunza
lugha ya Kiingerezaa, ushauri wa elimu, na habari kuhusu fursa za elimu
Marekani.
Amesema,
kituo hiko kilichopo maktaba kuu jijini hapa kitakuwa wazi kutumiwa na
wananchi wote bila malipo oyote na kitakuwa wazi kwa umma kwa siku za
Jumatatu hadi Ijumaa na jumamosi asubuhi hadi mchana.
Akifungua
kituo hicho, Naibu Waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia mhandisi
Stella Manyanya amesema, kituo hicho kitakuwa daraja la kuzifikia
taasisi za elimu ya juu za kimarekani, taasisi za utafiti na ufadhili wa
masomo.
Aidha aliumba ubalozi wa marekani kusaidia kujenga vituo vingine katika mikoa mingi nchini ili kusaidia elimu kwa umma.
Naibu
waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya
pamoja na Kaimu balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dk. Inmi
Patterson wakikata utepe kuashiria kufunguliwa kwa kituo cha Kimarekani
kilichoanzishwa kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani nchini
Tanzania pamoja na serikali ya Tanzania.
Naibu
waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya
akihutuba katika uzinduzi wa kituo cha Kimarekani kilichoanzishwa kwa
kushirikiana na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania pamoja na serikali
ya Tanzania. Kituo hicho kitakuwa kitovu cha uvumbuzi na ubunifu wa
teknolojia kitakachowawezesha wananchi kupata elimu na taarifa bila
vikwazo.
Kaimu
balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dk. Inmi Patterson akizungumza
kuhusu uzinduzi wa kituo cha Kimarekani kilichozinduliwa leo kuwa
kitakuwa kitovu cha uvumbuzi na ubunifu wa teknolojia kitakachowawezesha
wananchi kupata elimu na taarifa bila vikwazo.
Mkurugenzi Mkuu wa huduma za maktaba Tanzania, Dk. Alli Mcharazo
akielezea faida watakazozipata wananchi kwenye kituo hicho wakati wa
uzinduzi wa kituo cha Kimarekani kilichozinduliwa leo katika Maktaba ya
Taifa jijini Dar es Salaam.
Afisa
Uhusiano wa Ubalozi wa Marekani, Brinille Ellis akifafanua jambo wakati
wa uzinduzi wa kituo cha Kimarekani kilichozinduliwa leo katika Maktaba
ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wageni waalikwa waliofika kwenye uzinduzi wa kituo cha Kimarekani
kilichozinduliwa leo katika Maktaba ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Naibu waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella
Manyanya, akiweka sahihi katika ukuta wa kituo hicho kama ishara ya
kumbukumbu ya ufunguzi wa kituo hicho
Naibu waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya , mwenye suti nyeusi, Kaimu balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dk. Inmi Patterson,
katikati na Mkurugenzi Mkuu wa Huduma za Maktaba nchini Dk. Alli
Mcharazo wakipata maelekezo ya kituo kutoka kwa Afisa wa mambo ya
utamadui, Jeff Ladenson.
Naibu
waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya,
akifurahia jambo kutoka kwenye kitabu kinachopatikana ndani ya kituo
hicho, nyuma akishuhudiwa na Kaimu balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dk. Inmi Patterson.
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza wakati wa uzinduzi huo.
No comments:
Post a Comment