Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe
(katikati mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja ya Mkutano wa
MakatibU Wakuu kutoka Nchi Wanachama wa Kituo cha Afrika cha Sayansi ya
Jiolojia na Madini (AMGC). Wengine katika picha ni wawakilishi kutoka
Nchi wanachama pamoja Makamishna na Wakuu wa Vituo vya Madini.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe
(katikati) baada ya kufugua kikao cha Makatibu Wakuu kutoka Nchi
Wanachama wakiwa katika Kituo cha Afrika Sayansi ya Jiolojia na Madini
(AMGC). Wengine ni Kamishna wa Madini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka
(kushoto) na Assa Mwakilembe (kulia).
Baadhi
ya wawakilishi wa Bodi ya Kituo cha Afrika cha Sayansi ya Jiolojia na
Madini (AMGC), wa kwanza kutoka kulia ni Mwenyekiti wa UNECA, Dkt. Koja
Busia, Mwenyekiti wa Bodi, Masresha Gebreselassie, Mwenyekiti wa AUC,
Frank Mugyenyi na Mkurugenzi Mkuu wa AMGC, Ibrahim Shaddad.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe (anayeongea). Wengine ni washiriki katika kikao hicho.
Mshauri
Mwelekezi wa AMGC, Timo Gawronski akitoa maelezo kwa washiriki wa kikao
wakiwa katika maabara ya uchunguzi wa asili ya madini husika.
…………………..
Tanzania
imekuwa Mwenyeji wa Mkutano wa 37 wa Masuala ya Kisera ya Kituo cha
Afrika cha Sayansi ya Jiolojia na Madini (African Minerals and
Geosciences Center (AMGC) ambao unafanyika jijin Dar es Salaam.
Awali,
mkutano huo ulianza kwa kuwakutanisha Wakurugenzi wa Bodi ya kituo
hicho na kufuatiwa na mkutano wa tarehe 13 Agosti, 2017,
uliowashirikisha Makatibu Wakuu kutoka nchi Wanachama wa kituo husika.
Akizungumza
na Vyombo vya Habari wakati wa Mkutano wa Makatibu Wakuu, Kaimu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. James Mdoe alisema lengo la
kukutana ni kufanya tathmini na kuendeleza yale yaliyopangwa kutekelezwa
na nchi wanachama ikiwemo kupanga mipango ya mwaka ujao na bajeti ya
utekelezaji wa mipango hiyo.
Profesa
Mdoe alisema kuwa yapo mambo ambayo waliyokubaliana katika mkutano wa
36 yakiwemo ujenzi ya Maabara ya kisasa kwa ajili ya nchi za Maziwa
Makuu ambayo itasaidia katika shughuli za madini ikiwemo za uchunguzi wa
madini, kukiwezesha kituo hicho kufanya shughuli zake vizuri na
kusaidia nchi wanachama katika sekta husika.
Akizungumzia
manufaa ya kituo hicho nchini, alisema kuwa kituo hicho kimekuwa na
manufaa makubwa kwa Tanzania hususan Taasisi za Vyuo Vikuu nchini ambazo
zimekuwa zikikitumia Kituo hicho katika mafunzo mbalimbali.
“Sisi
tumepata bahati kubwa ya kuwepo kwa kituo hiki hapa nchini. Tayari vipo
Vyuo na wanafunzi ambao wamenufaika na uwepo wa kituo hiki. Kwetu sisi
ni faida kwa sababu hatutumii gharama kubwa za kufuata huduma
zinazotolewa na kituo hiki tofauti na nchi nyingine ambazo zipo mbali,”
alisema Prof. Mdoe.
Aidha,
alisema faida nyingine kwa nchi wanachama waliolipa ada kamili ni
kupata punguzo la asilimia 40 la kutumia maabara za Kituo hicho.Akizungumzia
malengo ya baadaye ya kituo hicho, alieleza kuwa ni kukifanya kuwa
kituo bora zaidi ikiwemo kuongeza idadi ya wanachama kutoka nchi nane
zilizopo sasa.
Hadi sasa nchi wanachama ni Tanzania, Msumbiji, Sudani Kaskazini, Ethiopia, Uganda, Kenya, Comoro na Angola.Sambamba na mkutano huo, itafanyika pia sherehe ya kuadhimisha miaka 40 ya kituo husika tangu kuanzishwa kwake.
No comments:
Post a Comment