Wadau wa habari nchini wameomba kupata taarifa iwe ni haki ya kila mtu ambayo inapaswa kulindwa kwa nguvu zote
na ni kiashiria kimoja wapo cha serikali yenye uwazi na inayothamini
mchango na ushiriki wa wananchi wake katika ujenzi wa taifa.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti, katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya
upatikanaji wa habari yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, wamesema kila
mtu ana haki ya kupokea na kutoa taarifa ili mradi tu asiende nje ya
swala husika.
Wamesema
kuwa, lengo la maadhimisho hayo ni kuongeza uelewa kwa wananchi juu ya
haki ya kila mtu na kupata taarifa muhimu kwa Maisha yao ikiwa ndani ya
hifadhi ya Serikali na kwingineko, namna viongozi waliyochaguliwa na
wanavyotekeleza majukumu yao.
Katika
maadhimisho hayo MISA-TAN walikabidhi tuzo kwa taasisi mbali mbali za
umma zinazotoa taarifa kwa uwazi na zile zinazobana taarifa. Kwa mwaka
2017, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeibuka mshindi wa kwanza
kwa utoaji na upatikanaji taarifa kwenye taasisi za umma na taasisi
iliyokuwa mshindi wa mwisho ni Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) baada
ya kubainika kuwa inabana taarifa. Kauli mbiu ya mwaka huu ni 'Kila
Mtanzania Anayo Haki Ya Kupewa Taarifa."
Mgeni
Rasmi Jaji Mstaafu na Mwenyekiti aliyepita wa Tume ya Haki za Binadamu
na Utawala, Amiri Ramadhani Manento, akifungua maadhimisho ya siku ya
kimataifa ya upatikanaji wa taarifa yaliyofanyika leo jijini Dar es
Salaam.
Wageni
waalikwa wakisimama kwa kuwakumbuka waandishi waliyopoteza maisha
katika maadhimisho ya kwanza Siku ya Kimataifa ya Upatikanaji wa Taarifa
yaliyofanyika leo Dar es Salaam, Tanzania.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa (CoRI), Kajubi Mukajanga akiakitoa
utangulizi kuhusu upatikanaji wa taarifa kwa wananchi nchini Tanzania
kwenye siku ya maadhimisho ya kimataifa ya upatikanaji wa taarifa leo
jijini Dar es Salaam.
Naibu
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Charles Stuart
akizungumza akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa
(hawapo pichani) kwenye siku ya Kimataifa ya Haki ya Kupata Taarifa
zinazoadhmishwa Septemba 28 kauli mbiu ya mwaka huu "Kila Mtanzania
anayo haki ya Kupewa Taarifa"
Makamu
Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Wakili James Malenga akizungumzia vigezo
vilivyotumika kuchagua taasisi zilizofanyiwa utafiti mwaka huu, Utafiti
uliofanywa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la
Tanzania (MISA-TAN) katika katika Siku ya Kimataifa ya Haki ya Kupata
Taarifa ambayo huadhimishwa kila mwaka Septemba 28.
Naibu
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Charles Stuart akikata utepe
wakati wa uzinduzi rasmi wa Chapisho la upatikanaji taarifa kwenye
taasisi za umma kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya upatikanaji
wa Taarifa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Kisenga LAPF jijini Dar es
Salaam.
Naibu
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Charles Stuart( wa pili
kutoka kulia) pamoja na wadau mbalimbali wakiwaonesha waandishi wa
habari pamoja na wageni waalikwa Chapisho la Upatikanaji Taarifa kwa
taasisi za umma kwa mwaka 2017.
Kaimu
Mkurugenzi wa MISA-Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akizungumza jambo
wakati wa uzinduzi wa Chapisho la Upatikanaji Taarifa kwa taasisi za
umma kwa mwaka 2017 lililofanyika leo jijini Dar Es Salaam.
Naibu
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Charles Stuart akionesha
kufuli la Dhahabu lililokwenda kwenye Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)
baada ya kubainika kuwa inabana taarifa kwa umma.
Naibu
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Charles Stuart akimkabidhi
tuzo ya Funguo la dhahabu Afisa Utafiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima Ya
Afya (NHIF), Shani Mussa walioibuka washindi wa kwanza upatikanaji
taarifa kwenye taasisi za umma.
Mwanazuoni
Mkongwe na Mwandishi wa habari nguli, Jenerali Ulimwengu akiongoza
majadiliano ya kuminywa kwa vyombo vya habari na asasi za kiraia kufanya
kazi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya upatikanaji wa taarifa leo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment