Naibu
waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla mapema jana Mei 28.2017 amekabidhi gari maalum la
kubebea wagonjwa (Ambulance) na vifaa vya Hospitali ikiwmo vitanda na
Magodoro katika Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga, Mkoani Pwani.
Dkt.
Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo, mbali na
kukabidhi gari hilo la wagonjwa na vifaa hivyo vya Hospitali kwa uongozi
wa Hospitali na Wilaya akiwemo Mkuu wa Wilaya na Mbunge wa Jimbo hilo,
aliweza kufanya ukaguzi wa ghafla kujionea mazingira ya Hospitali hiyo
na kubaini mapungufu mbalimbali ambayoo ametoa maagizo kupatiwa ufumbuzi
kabla ya kuchukuliwa hatua kwa uongozi wa Hospitali hiyo.
Naibu
waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akikata utepe wakati wa kukaabidhi gari la wagonjwa
hospitali ya Wilaya ya Mkuranga.
Miongoni
mwa changamoto hizo alizobaini katika Hospitali hiyo ni pamoja na kuwa
na mfumo mbovu wa uhifadhi wa taka, pamoja na uchafu katika wodi ya
wazazi jambo ambalo linaweza kusababisha hatari ya maambukizi kwa
Wagonjwa na wahudumu wenyewe wa Afya.
Awali
wakati wa kukabidhi gari hilo ambalo limenunuliwa kwa nguvu ya Madiwani
kwa kushirikiana na wadau mbalimbali pamoja na Mbunge wa jimbo hilo la
Mkuranga, Abdallah Ulega aliwataka kulitumia kwa uangalifu wa hali juu
huku likitakiwa kufanya shughuli zilizokusudiwa katika kusaidia wananchi
wake.
“Nimesikia
kileo chenu ambacho ni kupatiwa mashine ya X-Ray na na vifaa vingine
muhimu. Wizara yetu inalishughulikia hilo na tunawaomba muwe na imani na
Mbunge wenu ambaye amekuwa akinisisitiza juu ya jambo hilo. Hospitali
ya Mkuranga ni moja wapo ambayo itafaidika na msaada wa vifaa ikiwemo
mashine hiyo ya X-Ray” alisema Dkt. Kigwangalla wakati akizungumza na
wananchi mbalimbali ambao pia walipata fursa ya kuuliza maswali katika
tukio hilo.![](https://blogger.googleusercontent.com/img/proxy/AVvXsEiGQ40_e3I3UFAQmVGJdBncHC8TibFRTt_i-TD6v8O4HehLiaVScG0qq4Xm4MKkCemGjRAMN9BmKuAY3nOlInNUgfrKL8vRxGqH-9Ys0g9ZE_AKUukSkUFglNTV1IRwBQ86f53kKQTlVhfmGDJ5Odj3LxBCLv9UTdZEGJztpz4=)
Naibu
waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akikabidhi vifaa vya hospitali katika tuko la sherehe
hizo za kukabidhi gari la wagonjwa na vifaa vya hospitali ya Wilaya ya
Mkuranga.
Naibu
waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akiwa ndani ya gari la wagonjwa hospitali ya Wilaya
ya Mkuranga mara baada ya kulikabidhi
Naibu
waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akito maelezo namna ya chumba cha upasuaji kinatakiwa
kirekebishwe kufuata taratibu zake hospitali ya Wilaya ya Mkuranga.
Naibu
waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akiwa katika viunga vya hospitali ya Wilaya ya
Mkuranga.
Gari hilo la wagonjwa lililokabidhiwa.
Baadhi ya vifaa hivyo vilivuokabidhiwa.
No comments:
Post a Comment