Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda akiongeza na Balozi wa China
Nchini Tanzania Dr.Lu Youqing na ujumbe wake katika Viwanja vya Mnazi
Mmoja ambapo zoezi la upimaji wa Afya bure kwa wakazi wa Dar es Salaam
limeingia siku ya Nne.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda akizunguza na wananchi
waliojitokeza katika viwanja vya Mnazi Mmooja kwa ajili ya kupima afya
Balozi
wa Jamhuri ya watu wa China anaemaliza Muda wake nchini amemtembelea
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda katika Viwanja vya Mnazi
Mmoja ambapo zoezi la upimaji wa Afya bure kwa wakazi wa Dar es Salaam
limeingia siku ya Nne.
Mhe
Balozi wa China akiwa ameambatana na Maofisa wa Ubalozi huo hapa nchini
Ameshangazwa na UBUNIFU wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul
Makonda wa kuwasaidia wananchi wengi wa Mkoa kwa WAKATI MMOJA hususani
ni wenye vipato vya Chini ambao idadi kubwa hawawezi kumudu Gharama za
matibabu nje ya mifumo rasmi iliyowekwa na Serikali mfano wa Bima ya
Afya.
Kutokana
na Mkusanyiko huo wa Maelfu ya wananchi Mhe Balozi wa China amesema
Serikali ya Jamhuri ya watu wa China imeamua KUUNGA mkono jitihada za
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda na kuanzia sasa na
kuendelea serikali ya ya Jamhuri ya watu wa China itaungana na Serikali
ya Mkoa wa Dar es Salaam katika kusaidia zoezi upimaji Afya BURE kwa
kufanya yafuatayo :-
1.
Serikali ya China italeta Madaktari Bingwa kutoka China ambao wataungana
na Madaktari wa Timu maalum ya Mhe Makonda ambao wamekuwa wakitoa
huduma za upimaji Afya Bure hivyo Madaktari wa Tanzania wataungana na
Madaktari wa China katoka kuendesha huduma ya Utoaji wa Afya Bure Mkoa
wa Dar es Salaam.
2. Serikali ya China itatoa vifaa vya kisasa vya UPIMAJI ambazo vitasaidia kuongeza kasi ya upimaji kwa watu wengi zaidi.
3.
Serikali ya China ITAGHARAMIA dawa kwa watu wasio na UWEZO wa kumudu
Gharama za ununuaji dawa mara baada ya kupimwa na kuandikiwa dawa.
Mhe
Balozi wa China amewashukuru wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa
kumuunga mkono Mhe Makonda hatua ambayo imeishawishi serikali ya China
kusaidia katika zoezi hilo zuri lenye Malengo ya kutoa huduma bora za
Afya kwa Wananchi.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda AMEMSHUKURU
balozi wa China kwa Niaba ya wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa
kukubali kuunga mkono Jitihada za kuboresha Afya za wananchi wake,
ambapo amesema wazo hilo la kutoa HUDUMA ZA upimaji bure wa Afya
alilianza tangu akiwa Mkuu wa Wilaya ya KINONDONI, na kumuhakikisha
balozi huyo kuwa hilo litakuwa zoezi ENDELEVU kwa Mkoa wa Dar es Salaam
likiwa na Malengo makubwa matatu ambayo ni :-
1. Kuongeza UELEWA kwa Wananchi kuhusu umuhimu wa Upimaji wa Afya hata kama hawaumwi.
2.
Kuwawezesha wananchi WANYONGE kupata huduma za AWALI za upimaji wa Afya
ili kuwasaidia mapema katika hatua za AWALI kugundua matatizo yao.
3. Kubaini magonjwa ambayo husababisha VIFO katika hatua za AWALI.
Mhe
Makonda amesema kwa ujumla hatua anazozifanya Katia Sekta ya Afya
zinalenga kuunga mkono jitihada na kipaumbele cha Mhe Rais, Dkt. John
Pombe Magufuli katika masuala ya Afya, na ni kwa sababu hiyo ameamua
kuendelea kupambana na changamoto zilizoko kwenye Sekta ya Afya pasipo
kusubiria fedha za Bajeti ambazo hata hivyo hazitoshelezi mahitaji
halisi ya Afya kwa Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment