Pages

August 10, 2017

WAFANYAKAZI WA TANESCO KUPITIA TUICO WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KAMPENI YA "KA...TA" KWA KUONGEZA MAKUSANYO YA BILI ZA UMEME

 Mwenyekiti wa Kamati ya Majadiliano ya TUICO, Tawi la TANESCO, Bw. Hassan JM. Athumani, akizungumza wakati wa kutoa tamko la Wafanyakazi wa TANESCO kupitia chama chao cha TUICO kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kufuatia kampeni aliyoianzisha ya ukusanyaji wa madeni ya bili za umeme ijulikanayo kama "KA..TA". Tamko hilo alilitoa mbele ya wajumbe wa kamati kwenye ukumbi wa mikutano wa TANESCO makao makuu jijini Dar es Salaam, leo Agosti 10, 2017.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAFANYAKAZI wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kupitia chama chao cha TUICO, wamemponegza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kwa mchango wake mkubwa katika kuendeleza sekta ya umeme nchini ambapo kampeni yake ya “KA..TA” imekuwa na mafanikio makubwa ambapo wale wadaiwa sugu sasa wanalipa madeni yao.
Akitoa salamu za pongezi kwa Rais leo Agosti 10, 2017, kwenye makao makuu ya TANESCO Ubungo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Majadiliano ya TUICO, tawi la TANESCO, Bw.Hassan J.M Athumani, alisema, Mhe. Rais Magufuli, amewezesha TANESCO kukusanya madeni yake hata maeneo ambayo ilikuwa vigumu sana kulipa madeni.
“Wakati kampeni ya KA..TA ilipoanza mwezi Machi mwaka huu wa 2017, deni lilikuwa shilingi bilioni 275, kati ya hizo, taasisi za serikali pamoja na Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), zilikuwa zinadaiwa shilingi Bilioni 180 wakati taasisi binafsi, zilikuwa zinadaiwa shilingi Bilioni 95.
Bw. Athumani alisema ZECO pekee tayari wamelipa shilingi bilioni 18, wakati taasisi za serikali yakiwemo majeshi wamelipa deni shilingi Bilioni 18 pia, huku wadaiwa binafsi (private) wamelipa shilingi bilioni 5 na hivyo kufanya deni lililolipwa kufikia Julai 2017, kufikia shilingi bilioni 41.
“Kampeni hii ya rais ya KA..TA, imewezesha TANESCO sasa kukusanya bili za umeme hadi asilimia 104 kwa mwezi kutoka asilimia 90 kwa mwezi kabla ya kuanza kwa kampeni hii.” Alifafanua Mkuu wa Fedha wa TANESCO Bw.Philidon Siyame
Ilipoanza kampeni ya KATA, mwezi Machi, 2016. Deni lilikuwa Bilioni, 275, Serikali na taasisi zake ilikuwa inadaiwa bilioni 180, ilikuwa ni taasisi za serikali wakati private ilikuwa 95 bilioni.
Hadi Julai tumekusanya Bilioni 41, ZECO imelipa bilioni 18, taasisi zingine za serikali zikiwemo zile nyeti, zimelipa bilioni 18., wakati private wamelipa bilioni 5.
Akieleza zaidi kuhusu mchango wa Rais katika kuliwezesha Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, kupeleka huduma za umeme kwa wananchi, Mwenyekiti huyo wa TUICO-TANESCO, Bw. Athumani, alisema Shirika kwa sasa limefanikiwa katika uanzishwaji na uendelezwaji wa miradi ya kimkakati kama vile mradi mkubwa wa ufua umeme kwa gesi asilia wa Kinyerezi II Megawati 240, ambapo Mheshimiwa Rais aliweka jiwe la msingi mara tu baada ya kuingia madarakani mnamo Machi 16, 2016 na unaendelea kwa kasi na ifikapo Mwezi Desemba mradi huu utaingiza umeme katika Gridi ya Taifa, pia upanuzi wa mradi wa Kinyerezi I (Kinyerezi I Extension) utakaotoa Megawati 185.
Aidha Mwenyekiti huyo amemsifu Rais, kwa kuliwezesha Shirika la Umeme nchini TANSCO kutekeleza miradi mikubwa ya umeme kwenye maeeno mbalimbali nchini, ikiwa  ni pamoja na mradi mkubwa wa usafirishaji umeme wa msongo wa kilovoti 400 kutoka Mkoani Iringa hadi Shinyanga, Mradi mkubwa wa Gesi asilia wa Megawati 300 Somanga Fungu.
"Pia hivi karibuni ninyi ni mashahidi, serikali imesimamia uanzishwaji na uendelezwaji wa Mradi Mkubwa na muhimu kwa Taifa wa Rufiji Hydro Power Project wa Stieglers Gorge utakaofua zaidi ya Megawati 2,000 za umeme na kikubwa zaidi mradi huu utatekelezwa kwa fedha za ndani, kwa sisi wafanyakazi wa TANESC hiki ni kitu kikubwa sana na tuna kila sababu ya kumpongeza Mhe. Rais wetu." Aisisitiza.
Tunaamini kwa kasi hii umeme wa uhakika, Tanzania ya viwanda inawezekana. Alihitimisha kwa kusema.

 Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Majadiliano ya TUICO tawi la TANESCO, kutoka kushoto, Bw.Ahmed Mwinyi, ayewakilisha wafanyakazi upande wa uzalishaji umeme kwa njia ya mafuta (Themo Generation), Bw.Felix Lyimo, anayewakilisha wafanyakazi kutoak Kanda ya Dar es Salaam na Pwani na Bi.Asha Mtola, anayewakilisha wafanyakazi wanawake wa Shirika hilo wakisikiliza wakati tamko hilo likitolewa na Mwenyekiti wao. .

 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt.Tito Mwinuka, (wapili kushoto), Naibu Mkurugenzi Mtendaji (uwekezaji), Mhandisi Khalid James, (wakwaza kushoto) na baadhi ya wajumbe wa TUICO, wakinakili yaliyokuwa yakisemwa na Mwneyekiti wa TUICO Bw. Athumani.
 Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha (CFO), wa TANESCO ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya majadiliano ya TUICO, Bw.Philidon Siyame, (kushoto), Mwenyekiti wa TUICO-TANESCO, Bw. Hassan J.M Athumani, (katikati) na Kaimu Meneja Uhusiano TANESCO, Bi. Leila Muhaji, wakibadilishana mawazo baada ya mkutano huo.
 Bi. Leila Muhaji akizungumza kwenye mkutano huo.
 Bw.Siyame(kushoto) na Bw.Mwandu M. Chandarua, ambaye ni Katibu wa Kamati ya Majadiliano ya TUICO-TANESCO
 Mwenyekiti wa Kamati ya Majadiliano ya TUICO, Tawi la TANESCO, Bw. Hassan JM. Athumani, akizungumza wakati wa kutoa tamko la Wafanyakazi wa TANESCO kupitia chama chao cha TUICO kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kufuatia kampeni aliyoianzisha ya ukusanyaji wa madeni ya bili za umeme ijulikanayo kama "KA..TA". Katikati ni Katibu wa Kamati, Bw. Mwandu M.Chandarua, na Bw. Philidon Siyame.
 Naibu Mkurugenzi Mtendaji (uwekezaji), Mhandisi Khalid James(kushoto), akinakili, huku akiwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Mwinuka.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, (wapili kulia), Naibu Mkurugenzi Mtendaji (Uwekezaji), Meneja wa Mradi wa Kinyerezi I, Mhandisi Simon Jilima, (wakwanza kushoto) na mjumbe wa TUICO, Bw.Ahmed Mwinyi, wakiimba wimbo maarufu wa wafanyakazi, (Solidarity Forever).
Baadhi ya waandishi wa habari

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...