Mkuu
wa wilaya ya Newala, Aziza Mangosongo, akitembelea banda la VETA katika
maonesho ya Kilimo 2017 yanayoendelea mkoani Lindi katika viwanja vya
Ngongo ambapo alipongeza VETA kwa kuweka fursa nyingi za mafunzo ya
ujuzi kwa makundi mbalimbali ya wananchi. Aliahidi kushirikiana na VETA
ilikuwa wezesha wananchi wilaya ni kwake kunufaika pia na fursa
mbalimbali za mafunzo ya ufundi stadi.
Wanafunzi
wa shule ya sekondari Medi ya mkoani Mtwara wakipata maelekezo juu ya
aina ya mafunzo yanayotolewa katika vyuo vya ufundi Stadi walipotembelea
banda la VETA katika Maonyesho ya kilimo ya Nanenane yanayofanyika
kitaifa katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
.Mwalimu
wa Elektroniki wa Veta Kipawa, Aneth Mganga akiwapa maelezo wananchi
waliotembelea banda la VETA Pikipiki inayoendeshwa ni lazima dereva awe
amevaa kofiangumu.
Wananchi wakipata maelezo ya jiko la mafuta ya taa ambalo limebuniwa kwa kutotumia mafuta mengi na halina moshi.
Baadhi
ya wananchi waliofika kutembelea banda la VETA ili kuweza kupata
taarifa mbalimbali kuhusianana VETA pamoja na kuaangalia teknolojia
mbalimbali.
Na Chalila Kibuda,GlobuyaLindi
Katika
kukabiliana na changamoto za madhara ya ajali za pikipiki
yanayosababishwa na madereva kutovaa kofiangumu (helmet), Mamlaka ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imebuni teknolojia ya
kukabiliana na hilo.
Mwalimu
wa fani ya elektroniki kutoka VETA Kipawa, AnethMganga, amebuni mfumo
wa kielektroniki unaozuia pikipiki kuwa kampaka dereva awe amevaa
kofiangumu (helmet).
Akizungumza
na katika viwanja vya maonesho ya Nanenane Ngongo, mkoani Lindi,
mwalimu Aneth amesema mfumo huo ukianza kutumika na madereva wa pikipiki
utapunguza madhara endapo kunatokea ajali kwa kuwa bila ya kuvaa
kofiangumu pikipiki haiwaki na hata ukiwa katika mwendo ikitokea ukavua
kofiangumu pikipiki itazimika.
Aidha,
katika usalama barabarani inasaidia kuzuia wizi wa pikipiki kwani mwizi
hatoweza kuiwasha bila kofiangumu ambayo imeunganishwa kieletroniki.
Aneth
amesema anaendelea kufanya utafiti nakuboresha zaidi ubunifu huo, lakini
ameomba serikali na wadau mbalimbali kuunga mkono ili uweze kuenea,
kukubalikana kutumika na waendesha pikipiki katika maeneo mbalimbali
nchini.
No comments:
Post a Comment