Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa Water Aid Tanzania
kwa mwaka 2016-2021 wenye kauli mbiu "Kuweka Maji na Usafi wa Mazingira
kuwa kitovu cha Maendeleo"iliyofanyika kwenye hotel ya HyattRegency
jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Gerson Lwenge
wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa Water Aid Tanzania kwa mwaka
2016-2021 wenye kauli mbiu "Kuweka Maji na Usafi wa Mazingira kuwa
kitovu cha Maendeleo"iliyofanyika kwenye hotel ya HyattRegency jijini
Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mohamoud Thabit Kombo
wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa Water Aid Tanzania kwa mwaka
2016-2021 wenye kauli mbiu "Kuweka Maji na Usafi wa Mazingira kuwa
kitovu cha Maendeleo"iliyofanyika kwenye hotel ya HyattRegency jijini
Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akionyesha kitabu maalumu chenye mpango mkakati wa Water Aid
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassana leo amezindua Mpango Mkakati wa Water AID Tanzania .
Katika
mkutano huo uliofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es
Salaam na kuhudhuriwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi
Gerson Lwenge, Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo,
Mkurugenzi wa Water Aid Kanda ya Afrika Mashariki Bi. Olutayo Bankole
–Bolawole,Mkurugenzi WaterAid Tanzania Dkt. Ibrahim Kabole na wadau
mbali mbali wa maji, afya na mazingira.
Mpango
Mkakati wa miaka mitano wa Water Aid Tanzania wenye lengo la “ Kuweka
Maji Safi na Usafi wa Mazingira (WASH)” katika mipango ya Maendeleo ya
Jamii.
Makamu
wa Rais aliwapongeza Water Aid Tanzania kwa mpango wake huo, alisema
Maji ni rasilimali ambayo haijawahi kutosheleza mahitaji ya dunia na
hapa kwetu pia kwani kuna mahitaji makubwa ya maji kwa ajili ya shughuli
za kijamii, kiuchumi na kuhuisha na kutunza mazingira.
Vilevile
vyanzo vya maji vinaathiriwa sana na Ukame,kufurika n, kuvuruga
mtiririko asilia, mabadiliko ya hali ya hewa ongezeko la idadi ya watu
na viumbe wengine (Wanyama).
Mpango
wa Water Aid Tanzania wa miaka mitano utawezesha kuiweka Tanzania
kwenye ramani ya matumizi endelevu ya rasilimali ya maji na utachangia
katika utekelezaji wa malengo tuliyojiweka ya kupeleka huduma ya maji
safi na salama kwa wananchi kulingana na Sera yetu ya Maji na pia
kutekeleza ahadi tulizozitoa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya 2015.
Makamu
wa Rais alisema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbali mbali
imeendelea kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na
salama katika maeneo ya vijijini ambapo utekelezaji huo umeendelea
kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji vijijini ambapo kwa
mwezi Juni 2017 jumla ya watu 22,952,371 sawa na asilimia 72.58 ya
wananchi waishio vijijini wanapata maji safi na salama katika umbali
usiozidi mita 400 kama sera ya maji ya mwaka 2002 inavyoelekeza huku
katika Miji Mikuu ya mikoa kutoka asilimia 86 hadi asilimia 95, katika
miji mikuu ya Wilaya , miji midogo na miradi ya Kitaifa kutoka asilimia
60 hadi asilimia 75 na katika jiji la Dar es Salaam kutoka asilimia 72
hadi asilimia 95 ifikikapo 2020.
Makamu
wa Rais alisisitiza suala la usafi wa mazingira na kuhakikisha
tunalinda afya zetu tusishambuliwe na magonjwa ya milipuko kama vile
kipindu pindu na homa za matumbo. “Sote tunajukumu kubwa kuhakikisha
tunapata maji na kuzungukwa na Mazingira safi”.
Makamu
wa Rais aliwaagiza wanaohusika na usimamizi wa miradi ya maji na usafi
wa mazingira kuongeza jitihada zaidi ifikapo 2020 idadi ya wananchi
wanaopata maji iwe imeongezeka kufikia malengo tuliyojiwekea.
Mwisho,
Makamu wa Rais aliwashukuru wawakilishi wa mashirika yote ya Maendeleo,
wafadhili binafsi na Watendaji wengine ikiwa pamoja na Sekta Binafsi na
Taasisi za Kidini ambazo zimesaidia katika upatikanaji wa huduma za
maji na usafi wa mazingira na kuboresha mazingira.
No comments:
Post a Comment