Naibu
Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikata utepe na kuweka
jiwe la msingi katika shule ya sekondari Nyamtinga wilayani Rorya.
Baadhi ya vyumba vya madarasa vilivyokaguliwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa
Rorya na kuwapongeza kwa ujenzi wa madarasa na mabweni.
Mbunge wa Vitimaalum Agnes Marwa akizungumza na wananchi wakati wa ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo.
....................................................................................................................................................
Naibu Waziri
Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo amewapongeza viongozi na
watendaji wa wilaya na halmashauri ya wilaya ya Rorya kwa mahusiano
mazuri waliyonayo katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Jafo alitoa sifa hizo alipokuwa wilayani humo kwa ziara ya kikazi ya kukagua miradi na kuongea na watumishi
Katika ziara
hiyo, Jafo alifanikiwa kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa, mabweni,
maabara, na vyoo kwa sekondari ya Nyamtinga na Nyamunga ambapo majengo
hayo yamebainika kujengwa kwa ubora wa kuridhisha.
Ujenzi wa miundombinu hiyo imegharimu zaidi ya sh.milioni 500 kutoka serikali kuu kwa lengo la kuboresha elimu hapa nchini
Kwa upande
wake,Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara, Agness Marwa amempongeza Naibu
Waziri huyo kwa kufika wilayani Rorya na kwamba amekuwa Waziri pekee
aliyefanikiwa kutembelea wilayani humo katika kipindi hiki cha serikali
ya awamu ya tano.
Mbunge huyo ameishukuru serikali kwa upendo wake wa kuisaidia wilaya hiyo miradi ya maendeleo.
Naibu Waziri
Jafo leo amekamilisha ziara yake ya kikazi ya siku sita ya kukagua
miradi ya maendeleo na kuongea na watumishi kwa mkoa wa Kagera na Mara
na anaendelea na ziara yake katika mikoa mingine.
No comments:
Post a Comment