Pages

August 8, 2017

COSTECH ILIVYOWANOA MAOFISA UGANI WA MKOA WA LINDI KATIKA MAONYESHO YA NANENANE


 Mwezeshaji kutoka Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Dk.Emmarold Mneney (kulia), akitoa mafunzo ya siku moja ya kilimo chenye tija  kwa maofisa Ugani wa Mkoa wa Lindi kwenye Maonyesho ya Kitaifa ya Nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya Ngongo mkoani hapa juzi.

 Ofisa Kilimo kutoka Manispaa ya Lindi, Amina Pemba akizungumza kwenye mafunzo hayo.
 Maofisa Ugani wakipata mafunzo.

Ofisa Kilimo kutoka Manispaa ya Lindi, Hussein Mwapili, akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake baada ya kupata mafunzo hayo.

 Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Philbert Nyinondi ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Morogoro (SUA), akizungumza na maofisa ugani hao katika mafunzo hayo.
 Mafunzo yakiendelea.
 Wahamasishai wa matumzi ya Bioteknolojia katika kilimo wakijadiliana wakati wa mafunzo hayo. Kulia ni Happiness John na Flaviana Anthony.
Ofisa Mifugo na Uvuvi wa Wilaya ya Kilwa, Ramadhan Hatibu akizungumza kwenye mafunzo hayo.

Na Dotto Mwaibale, Lindi

MAOFISA ugani mkoani Lindi wamesema wanashindwa kuwahudumia kikamilifu wakulima kutokana na kukosekana kwa usafiri wa kuwapeleka vijijini pamoja na kutelekezwa na 
wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa kushindwa kuwapatia mafunzo ya mara kwa mara.

Wakizungumza juzi katika mafunzo kuhusu kilimo bora yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, COSTECH, maofisa ugavi hao walisema kutokana na 
upungufu wa wataalam hao wamekuwa wanahudumia vijiji vingi na mtu mmoja anaweza kuhudumia vijiji hadi sita. 

Pia walisema kwamba tatizo lignine wamekuwa hawapati 
mafunzo ambayo yatawezesha waweze kwenda na wakati.

Ofisa Ugani kutoka Manispaa ya Lindi Hussein Mwapili alisema wizara ya kilimo baada ya kuwakabidhi maafisa ugani kwa halmashauri imeshindwa hata kuwafuatilia na hata kuwajengea nyumba wakati wizara zingine kama elimu na afya zinawakumbuka wataalamu wao kwa kuwajenge nyumba na kuwapa miongozo ya mara kwa mara.

“Sisi tumesahulika kabisa, tunakumbukwa wakati wa njaa tu ndipo utaona tunalaumiwa kwamba tunaishi mjini, lakini wizara ya kilimo imefanya nini kuhakikisha maafisa ugani wanaishi katika mazingira bora ya kufanyia kazi? Kule vijiji tunaambiwa 
tukaishi huko je kuna nyumba za wagani? alihoji.

Amina Pemba ambaye ni afisa ugavi kutoka manispaa ya Lindi alitaja changamoto zinazowakabili ni kukaa kwa muda mrefu bila kupata mafunzo au semina kuhusu taaluma yake ya kazi kwa vile kilimo ni sayansi na inabadilika mara kwa mara.

Alisema hata kama anatembea kwa miguu hawezi kuwafikia watu wengi alisema maafisa ugavi hawana usafiri wa kwenda vijijini. “Tunashukuru juzi mkurugenzi ametupatia gari idra ya kilimo, hatujawahi kupatiwa usafiri tangu nianze kazi miaka 20 
iliyopita.”

Alisema maofisa ugavi hawana vifaa vya kupimia ardhi kujua aina ya madini yaliyoko pale ili waweze kuwashauri wakulima aina ya mazao anayotakiwa kupanda au aina ya mbolea anayotumia kulingana na hali ya udongo.

Pemba alisema kwamba hata tafiti zinazofanywa na wataalamu wa wizara ni taasisi zingine za utafiti hazishuki kwa maafisa ugavi jamboa mbalo linafanya tafiti hizo zisiwe na msaada kwa mkulima.

Alisema pamoja  na kuhamasishw akwenda vijijini lakini hakuna nyumba za maafisa ugavi na hilo linatokana na wizara ya kilimo kuwatekeleza wataalamu hao na hivyo kusababisha kufanya kazi katika mazingira magumu.

“Sisi tukiwezeshwa wagani tutawajibika, lakini kwa hali ilivyo sasa ni ngumu kuwafikia wakulim wote, wagani wengi hawana usafiri,” alisema.

Ofisa ugani wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Mligo Eisen   alisema katika idara ya mifugo kuna pikipiki tatu na idara yote ya kilimo kuna gari moja ambalo tangu lipatikane halina zaidi ya miezi sita na vifaa hivyo vya moto ndivyo vinavyotegemewa na maofisa ugani na maofisa mifugo ili kuwafikia wakulima hali 
ambayo ni changamoto kubwa.

Aliongeza kuwa changamoto nyingine ni uhaba wa maofisa ugani jambo linalochangia wakulima kupata elimu ya kilimo kwani ofisa ugani mmoja anatakiwa kutembelea vijiji vitatu na kukutana na wakulima wa aina tofauti ambao wanalima mazao 
tofauti.

Alisema hali hiyo inamfanya ofisa ugani husika kushindwa kuwafikia wakulima wake wote hivyo kuwa chanzo cha wao kukosa elimu ya kilimo na kupata chakula kidogo na 
mazao ya biashara.

Katika maonesho ya nanenane yanayoendela mjini hapa, wakulima ambao wamekuwa wanapatiwa mafunzo na tume ya taifa ya sayansi na teknolojia wamekuwa wanawalalamikia wagani wa kilimo kwa kushindwa kuwafikia na kuwapatia huduma za 
ushauri wa kitaalamu wanazohitaji.




No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...