Pages

August 6, 2017

BWANA NELSON PALLANGYO NA BI. THERESIA BYAKWAGA WAFUNGA NDOA MJINI KARATU

 Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kaskazini, Jimbo La Karatu, Usharika wa Karatu Mjini akiwafungisha ndoa Bw. Nelson Charles Pallangyo na Bi. Theresia Justine Byakwaga iliyofanyika Agosti 5, 2017 na baadae sherehe ikafanyika ukumbi wa Samawe Complex. PICHA ZOTE NA KAJUNASON/MMG - KARATU.
Bwana Harusi Nelson Charles Pallangyo  akimvalisha pete mkewe Bi. Theresia Justine Byakwaga wakati wakifunga ndoa katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kaskazini, Jimbo La Karatu, Usharika wa Karatu Mjini akiwafungisha nd Agosti 5, 2017.  Bibi Harusi Theresia Justine Byakwaga akimvalisha pete mumewe Nelson Charles Pallangyo wakati wakifunga ndoa katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kaskazini, Jimbo La Karatu, Usharika wa Karatu Mjini akiwafungisha nd Agosti 5, 2017.
Bwana Harusi Nelson Charles Pallangyo na mkewe Bi. Theresia Justine Byakwaga wakila kiapo cha uaminifu wakati wakifunga ndoa yao takatifu. Pembeni ni wasimamizi wao.
 Waumini wakifuatilia ibada.
  Mchungaji akiwagawia vyeti.
 Maharusi wakionyesha vyeti vyao mara baada ya kufunga ndoa. Pembeni ni wasimamizi wao.
 Maharusi wakitoka kanisani.
 Wazazi wa Bwana Harusi (kushoto), Charles Pallangyo na Bibi Harusi (kati mwenye shati la blue) Justine Byakwaga wakizungumza machache na mchungaji mara baada ya kufungisha ndoa ya watoto wao Nelson Charles Pallangyo na Bi. Theresia Byakwaga.
 Pongezi za ndugu, jamaa na marafiki mara baada ya kutoka kanisani.
 Pongeni na shamra shamra zikiendelea.
 Bwana Harusi Nelson Charles Pallangyo na Bibi Harusi Theresia Justine Byakwaga wakiwa katika picha ya pamoja na wazazi wa pande zote mbili.
   Wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wakiwa katika picha ya pamoja na maharusi.
Maharusi wakikaribushwa nyumbani kwa shangwe na vigelegele....

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...